KUWA NA SHAHADA HAIMAANISHI MAISHA YATAKUWA MAZURI
Inawezekana
umeshangazwa na kichwa cha habari, hata mimi ninashangaa kwanini
nimefikiria hivyo. Baada ya kufikiria kuhusu elimu na maisha mazuri
nikakumbuka kitu kimoja kutoka kwa mwandishi mmoja hivi, alisema kuwa
“Elimu ni ufunguo wa maisha”. Suala ni kwamba kuwa na ufunguo umamaliza
kila kitu, bali unaweza kuwa na ufunguo usijue ni wakufungulia wapi au
nyumba gani. Je wewe una ufunguo wa maisha?
Ukija
kwenye mfumo wetu wa elimu ni wa kukuelimisha au kukufanya ujue habari
ya vitu fulani katika historia yetu na Lugha yetu na taaluma mbalimbali.
Lakini ni mara ngani tumekuwa na wasomi wasiokuwa na mwelekeo wa
maisha? Tunao wengi na wengine ni ndugu zetu, Hivyo elimu yao ni ufunguo
wa maisha au kufuri la maisha?
Ninachotaka
kukigusia ni kwamba elimu ya darasani sio pekee itakayokusaidia kuishi
maisha ya huku mtaani, unahitaji elimu ya mazingira yanayokuzunguka.
Shahada yako ni nyenzo tu ya kukuvuta na kukuweka kwenye fulsa fulani
ila unahitaji ujuzi wa ziada katika kuishi maisha yanayostahili.
Usishangae
kuona watu ambao wanaongoza kwa kuomba rushwa ni hao hao tunaosema wana
elimu nzuri, tatizo ni nini? Watu wa elimu ya kati ndio wamekuwa
wakimiliki uchumi kwa sehemu kubwa, kwakuwa wao hawaishi kutumia cheti,
wanaishi kwa kutumia ujuzi walionao kufanya vitu wanavyofanya na hata
kufanikiwa kuliko watu waliokwenda shule. Maisha mazuri ni mchanganyiko
wa vitu vingi pamoja na elimu ya darasani , elimu ya mazingira
yanayokuzunguka na ujuzi wa maisha kutoka vizazi vilivyopita.
Je
wajua watu wanaomiliki makampuni makubwa ambayo inawezekana na wewe
umeajiriwa huko, hawana elimu kubwa kuliko unavyofikiri ila wamekuajiri
wewe wenye elimu uwatumikie? Je siri ni nini? Tafakari na uchukue hatua.
Kuwa
na shahada inakupa fursa au upenyo wa kuingia sehemu fulani. Kama
shahada inakupa upenyo wa kuingia au kukubalika sehemu fulani ila maisha
mazuri yatategmea jinsi gani unavyotumia elimu ya darasani na ile ya
mazingira yanayokuzunguka kufanyikisha malengo ya maisha yako.
Hivyo
unapotumia elimu yako na kufanya kitu au mambo sahihi mafanikio yako
sahihi yanaonekana, na vile vile unapotumia elimu yako kufanya mambo
ambayo si sahihi utapata mafanikio ambayo si sahihi kwakuwa kuna kitu
kimejificha kwenye mafanikio yako. Suala linakuja hivi je Kizazi kijacho
kitaweza kuendeleza hayo mafanikio?
0 comments: