MWANAFUNZI AUA WATU SITA KWA WAKATI MMOJA, NI MTOTO WA MTAYARISHAJI MAARUFU WA FILAMU


Polisi
nchini Marekani wamethibitisha kuwa kijana Elliot Rodger mwenye miaka 22
ambaye ni mtoto wa mtengeneza filamu maarufu, ndie aliyefanya mauaji ya
watu sita kwa pamoja jijini Califonia.
Kijana
huyo ambaye ni mwanafunzi ni mtoto wa Peter Rodger ambaye ni
mtayarishaji filamu wa Marekani aliyesaidia kutengeneza filamu ya The
Hunger Games.
Polisi
wamesema kuwa kijana huyo aliwachoma visu wanafunzi watatu aliokuwa
akishare nao chumba kwenye nyumba yake ambapo baadae alikwenda katika
duka moja na kuanza kurusha risasi mfululizo zilizojeruhi watu na
kusababisha vifo.
Baada ya
tukio la kurushiana risasi na polisi Rodger alikutwa amekufa ndani ya
gari lake lililopata ajali akiwa na majeraha kadhaa ya risasi kichwani.
0 comments: