LISSU AWALIPUA MAWAZIRI NA WABUNGE kwa kugeuka ombaomba

Mbunge
wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana amewalipua
baadhi ya mawaziri na wabunge kwa kugeuka ombaomba katika mifuko ya
hifadhi ya jamii.
Akizungumza
bungeni jana katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa
mwaka 2014/15, Lissu alisema kuwa atawasilisha hoja binafsi katika Ofisi
ya Spika ili iundwe tume kwa ajili ya kuwachunguza wabunge na mawaziri
hao.
Huku
akionyesha baadhi ya nyaraka ambazo wabunge hao wameiandikia mifuko
hiyo ya jamii kuomba fedha, Lissu alisema kitendo hicho kimewafanya
viongozi hao kusifia kila jambo linalofanywa na mifuko hiyo, hata kama
ni baya.
Lissu
alitoa kauli hiyo huku wabunge watano kati ya wanane waliomtangulia
kuchangia mjadala huo, kuisifia mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, huku
wakimtaja kwa jina Mkurugenzi wa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Ramadhan Dau kwamba ni mfano wa kuigwa.
“Sifa
hizi zina sababu yake. Kuna nyaraka na barua zinazoonyesha wabunge
mbalimbali waliochukua fedha za mifuko hii kwa sababu mbalimbali,”
alisema Lissu na kuongeza;
“Naomba baadaye Bunge liunde kamati teule ili kuichunguza mifuko hii na viongozi hawa.”
Hata
hivyo, Lissu hakumalizia hoja yake hiyo baada ya muda wake wa kuchangia
kumalizika na kutakiwa kukaa chini na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan
Zungu.
Wahusika
Baada
ya kuahirishwa kwa kikao hicho cha Bunge, Lissu alilionyesha gazeti
hili nyaraka za vigogo hao zikionyesha wote wameomba kati ya Sh500,000
hadi Sh10 milioni.
Kati
yao wapo mawaziri, naibu mawaziri ambao wameomba fedha hizo kwa ajili
ya matumizi mbalimbali, huku baadhi yao wakieleza kuwa fedha hizo ni kwa
ajili ya kufanya shughuli za maendeleo katika majimbo yao, ikiwa pamoja
na kununua jezi na mipira.
Sakata
hilo pia linaihusisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, ambapo kigogo mmoja wa wizara hiyo (jina tunalo) ameomba
mfuko mmoja wa jamii kumnunulia vifaa vya ofisi ikiwamo kompyuta kwa
ajili ya matumizi ya wizara.
“Unaweza
ukajiuliza maswali mengi. Wizara inaomba fedha katika mfuko wa jamii
ili kununua kompyuta na vifaa vingine vya ofisi wakati ina bajeti ya
ununuaji wa vifaa hivyo.
CHANZO:MWANANCHI
0 comments: