RAIS WA BOLIVIA ‘EVO MORALES’ ASAJILIWA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA
Rais Evo Morlaes
Rais
wa serekali ya Bolivia ‘Evo Morales’ amekubali kusajiliwa na timu ya
Sport Boys ya ndani ya nchi hiyo na kucheza soka la kulipwa.
Morales,
mwanasoka wa siku nyingi amekubali kusajiliwa na klabu ya Sports Boys
ya nchini mwake kwa ajili ya msimu ujao wa soka. Morales amesajiliwa na
klabu hiyo yenye makazi yake katika Jimbo la Kusini Mashariki mwa nchi
la Santa Cruz. Klabu hiyo imesema kwamba Rais Morales atakuwa akicheza
walau dakika 20 kwenye mechi, kutokana na kazi zake nyingi za kuongoza
nchi.
Morales (54) atakuwa akilipwa kima cha chini cha mshahara cha pauni 127 na klabu hiyo ya daraja la kwanza.
“Anapenda
soka na pia anaweza kucheza vizuri, atavaa jezi namba 10. Tutamtumia
orodha ya mechi zetu na yeye atachagua zile ambazo atapata nafasi,”
akasema Rais wa Klabu ya Sport Boys, Mario Cronenbold.
Source:BBC
0 comments: