JE WAJUA JINSI YA KUONGEZA MVUTO KWA MPENZI WAKO SOMA HIII HAPAAA..
Kama
umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako
alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa
sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.
Ukiwa kwenye
ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea
huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia.
Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake
kwa kasi sana.
Itafikia
hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na
kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha.
Hisia kwamba hamuendani humwingia.
UNAFANYAJE SASA?
Kubwa
unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka
thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako
hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.
Tayari
tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa
nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu
zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.
ANZIA MWANZO
Ni rahisi
zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari
mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi
zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni
mambo gani hayo? Twende hapo chini.
CHUNGA KAULI ZAKO
Naomba
ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu
cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa
mpenziwe ni kupima sana kauli zake.
Acha
kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo
huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini
zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja
sana.
Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.
USIRUHUSU MAPENZI
Msichana
mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu
mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na
usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.
Mpe hoja;
kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza
kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza
kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana
na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa
asilimia kubwa.
Ukumbuke
kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na
uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo
hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!
SOMA HABARI NYINGINE HAPA>>>>http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/
0 comments: