NDEGE YA MALASIA YAPOTEA NA ABIRIA 239

Ndugu wa
abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo wakisubiri taarifa kuhusiana na ndege
hiyoNdege ya Malaysia Airlines iliyokuwa na abiria 227 na wafanyakazi
12 inahofiwa kuanguka huko katika bahari kusini mwa China, kwa mujibu wa
shirika la habari la serikali la Vietnam.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777-200ER iliyokuwa inatoka Kuala Lumpur
kuelekea Beijing, ilikuwa imepotea kwa masaa kadhaa. Kama ripoti hiyo
ikithibitisha, itakuwa ni ajali mbaya ya ndege ya aina hiyo (Boeing 777)
tangu iingie sokoni miaka 19 iliyopita.

Ndugu wakifanya mawasiliano kutaka kujua ukweli
Malaysia Airlines bado haijathibitisha iwapo ndege hiyo imeanguka.
0 comments: