WAANDISHI WA HABARI WACHINJIWA BAHARINI ... JUA ZAIDI KWA KUSOMA HAPA
HATIMAYE kifungu cha 57 fasihi ndogo ya 3 inayozungumzia nafasi ya
waandishi wa habari kuruhusiwa kuingia katika vikao vya kamati ya Bunge
Maalum la Katiba imepitishwa na wabunge wa CCM huku wabunge wa Chadema
akiachwa pasipo kujua cha kufanya.Hatua hiyo ni sawa na waandishi wa
habari kuchinjiwa Habarini huku wananchi wakinyimwa uhuru wa kupata
habari kuhusu mambo yatakavyo endelea ndani ya vikao vya Bunge hilo.
Katika kile kinacho onekana kwamba ni njama za kuweka mambo katika hali ya usiri zaidi, katika mkutano wa Bunge Maalum la Katiba Mpya inayoendeloe mjini Dodoma, inaonyesha ni jinsi gani wabunge wa CCM walijipanga kufanya mambo kwa usiri na kuwanyima wananchi fulsa ya kujua mambo yanavyo endelea ndani ya vikao vyao.
Awali suala hilo lilileta mvutano mkubwa ndani ya bunge hilo.Hatua hiyo imekuja kutokana na misimamo ya wabunge wa CCM waliowengi ndani ya Bunge kutaka waandishi wa Habari watungiwe kanuni za kuwakataza kuingia katika vikao vya kamati za bunge hilo kwa madai kwamba wanatabia ya kuandika uongo.
Akizungumzia suala hili Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya rasimu za kanuni za bunge hilo George Simbachawene alipinga suala hilo kwa nguvu zote huku pia akipingana hata na maamuzi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Professa Costerick Mahalu ambaye alitaka suala hilo liachwe wanza ili kamati yake ikaangalie namna nzuri ya kuwaruhusu wanahabari kuingia katika vikao hivyo.
Kitendo cha Simbachawene kushikilia msimamo huo inaleta tafisiri kwamba huo ndiyo mpango wa Chama Cha Mapinduzi uliokuwepo tagu mwanzo ya kuwataka wabunge wake walijipange kufanya mambo yanayopaswa kuwa siri yafanyike kwa uwazi na yake yaliyopangwa kufanyika kwa uwazi yafanyike kwa usiri bila kujali kwamba wanavunja Katiba mama ambayo bado inatumika mpaka hivi sasa.
Awali CCM ilibuka na hoja ya kwamba kura zipigwe kwa uwazi huku wakijua kwamba katiba hairuhusu kura yoyote kupigwa kwa uwazi, bali kura zote zinapigwa kwa siri,lakini katiba hiyo hiyo katika Ibara ya 18 kina sema kwamba "Kila mtu anayo haki ya kutoa na kupokea ama kupewa habari"sasa iweje CCM itake kuweka mazingira magumu kwa watanzania kupata,kutoa ama kupewa habari za mikutano ya kamati za bunge linalohusu katiba ya wananchi wote?.
Hoja za kuitaka bunge hilo kufuta mapendekezo ya kanuni katika kifungu cha 51 na 57 fasiri ndogo ya 3 inayompa mwenyekiti wa kamati haki ya kutoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu kilichozungumzwa na kamati, badala ya kuruhusu waandishi waingie na kusikiliza kinachojadiliwa wenyewe na kuwaeleza wananchi wengine ilipigwa na Wabunge Halima Mdee Chadema ,Amos Machari NCCR-Mageuzi,Ester Bulaya CCM,Maria Sarungu na Ezekiel Oluoch wote wateule wa Rais Kikwete.

0 comments: