SERIKALI YATANGAZA KUAJIRI WALIMU 36,000 MWEZI HUU....WALIMU HAO WATATAKIWA KURIPOTI KATIKA VITUO VYAO VYA KAZI APRILI MOSI MWAKA HUU
Serikali imetangaza kuwajiri walimu wapya 36,071 mwaka huu ambao majina yao yanatarajia kutangazwa katikati ya mwezi huu (Machi) na watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo vyao vya kazi Aprili mosi mwaka huu.
Naibu
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim
Majaliwa, aliyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha
Kumepambazuka jana kinachorushwa na Radio One.
Majaliwa
alisema walimu hao watapangiwa katika vituo mbalimbali vya kazi kuanzia
Aprili Mosi, mwaka huu na majina yatatoka katikati ya mwezi huu.
Alisema
kati ya walimu hao watakaoajiriwa, 36,020 wataajiriwa na halmashauri za
wilaya ambao ni walimu wa shule za msingi na sekondari na 51 watakuwa
chini Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya
vyuo.
Aliongeza kuwa kati yao, walimu wa stashahada ni 17,028 na 5,416 ni wa shahada kwa ajili ya sekondari na 12,677.
Alifafanua
kuwa wanaoajiriwa ni wale waliohitimu hivi karibuni katika vyuo vya
ualimu na walimu wa masomo ya sayansi watapewa kipaumbele.
Majaliwa
alisema tayari Wizara imewaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri na
maofisa elimu kupitia ikama ya walimu kubaini shule zenye upungufu wa
walimu ili walimu hao wapya wanaoajiriwa wapelekwe huko hususani katika
shule zilizopo vijijini.
Alisema
kuajiriwa kwa walimu hao kumepunguza tatizo la upungufu wa walimu
21,684 baada ya ajira hiyo na kwamba hata hivyo upungufu mkubwa kwa
walimu wa sayansi ni 26,212.
Alisema
serikali imeweka mkakati wa kukabiliana na tatizo la punguza wa walimu
wa sayansi kwa kuwachukua wanafunzi waliohiotimu vyuo vikuu ili
wapelekwe kwenye vyuo vya ualimu.
Kuhusu
tatizo la baadhi ya walimu kukimbia vituo vya kazi, alisema kimsingi
sheria ipo wakishaajiriwa wanakuwa katika kipindi cha matazamio cha
miaka mitatu na wanafanyiwa ukaguzi na wakaguzi ili kubaini kama wana
uwezo wa dhati.
0 comments: