KAULI YA WAZIRI WA ELIMU YAWACHEFUA WALIMU JUA HAPA NI NINI HASA
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimekerwa na kauli ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa , kuwa serikali inaendelea kujadiliana na taasisi za fedha juu ya namna ya kulipa deni la malimbikizo ya mishahara ya walimu yanayofikia Sh. bilioni 61.
CWT
imesema kauli hiyo ya serikali ni kutafuta visingizio baada ya
kushindwa kutekeleza ahadi yake kuwa ifikapo Februari, mwaka huu deni la
walimu litakuwa limelipwa.
Rais wa CWT, Gration Mkoba, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Alisema
majadiliano ya mishahara ya walimu yalitokana na mgomo wa 2012 baada
ya kukaa kwenye meza ya majadiliano na serikali ilikubali kulipa deni na
kuandaa utaratibu wa kupandisha walimu madaraja.
“Inasikitisha
kuona majadiliano yanahusisha waandishi wa habari bila ya kujua kuwa
kwa kauli yake waziri tayari walimu wameingia kwenye mgogoro na
serikali, lakini nawasihi walimu wasubiri tamko rasmi la mgogoro,”
alisema.
Mkoba
alisema tangu serikali ilipoahidi kutekeleza madai yao, hakuna hata dai
moja lililotekelezwa lakini imewashangaza kuona ikijinadi kuwa
inaendelea na majadiliano ya kulipa deni hilo wakati majadiliano hayana
tija kwa mwalimu.
Alisema
Novemba, mwaka jana mkutano mkuu wa CWT ulitoa siku 60 kwa serikali
kukamilisha taratibu zote la kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu
nchini.
Pia
Januari mwaka huu kwenye kikao cha Baraza la Taifa la CWT kiliazimia
kuwa ifikapo mwishoni mwa Februari, mwaka huu, ikiwa serikali itashindwa
kulipa malimbikizo hayo litakuwa tayari kuongoza mgomo.
CHANZO: NIPASHE
0 comments: