Kocha wa Nigeria Keshi amejiuzulu
Kocha wa Nigeria Keshi amejiuzulu
Kocha wa Nigeria coach Stephen Keshi amejiuzulu wadhfa wake katika timu hiyo .
Keshi
amejiuzulu punde baada ya timu ya Super Eagles kuondolewa kutoka kwenye
kipute cha kombe la dunia ilipolazwa 2-0 na Ufaransa .
Nahodha
wa timu hiyo Joseph Yobo aliyejifunga bao la pili la Ufaransa naye pia
ametangaza kustaafu .Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alichukuwa
wadhfa huo mwaka wa 2011 na akaiongoza timu hiyo kufutwaa ubingwa wa
afrika mwaka uliopita .
Hii
haitakuwa mara ya kwanza kwa Keshi kujiuzulu wadhfa wakae,mwaka wa 2013
Keshi alikuwaradhi kujiuzulu lakini akashawishiwa kusalia kama kocha na
waziri wa michezo wa Nigeria.
Chini ya
uongozi wake Super Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika mkondo wa
pili wa kombe la dunia tangu mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa na migomo
ya mara kwa mara ya wachezaji wake wakidai malimbikizi ya marupurupu
yao.
Kuondoka kwake kumefikisha idadi ya wakufunzi waliojiuzulu kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia kutimia makocha 6.
Makocha
wengine waliondoka ni pamoja na Luis Suarez, wa Honduras, Carlos Queiroz
wa Iran's , Alberto Zaccheroni wa Japan , Cesare Prandelli wa italia na
Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.
Keshi, aliwahi kuhudumu kama kocha wa Mali na Togo.
0 comments: