RAIS JOYCE BANDA AMEAMURU KUSITISHWA KWA ZOEZI LA KUHESABU KURA, NA KUTAKA UCHAGUZI URUDIWE

Baadhi ya viongozi wanaowania urais nchini Malawi
Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya
kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
ulifanyika jumanne iliyopita.
Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe muda mfupi uliopita ameiamuru Tume ya
uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe
ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba yeye hatogombea tena urais wa
nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr
Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile
alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji
kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema
kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia
uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya
nchi.
bbc
0 comments: