OFISI YA RAIS-SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,324 30 JUNI, 2014.
Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,324.
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia
Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,324
ambazo ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Katibu wa Sekretarieti
ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi 1,334 zimeainishwa bayana
kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ili kuwawezesha wahitimu wote wenye sifa na uwezo kutuma maombi kwa ajili ya kujaza nafasi hizo ajira Serikalini.
"Nadhani ni
vizuri zaidi kwa kila muhitimu anayetafuta kazi serikalini kufungua
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuangalia nafasi za kazi zilizotangazwa
na pale anapoiona kazi inayoendana na sifa alizonazo kutuma maombi yake
ili kuweza kushindanishwa na wengine....maana ajira za Serikali hivi
sasa ni za ushindani hivyo inampasa kila anayetaka kupata kazi
serikalini kujiandaa vyema ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya
kuajiriwa katika Utumishi wa Umma" alisema Daudi.
Alifafanua
kuwa kwenye tovuti hiyo kuna matangazo mawili tofauti ya kazi ambapo
moja liko katika lugha ya Kingereza likiwa na jumla ya nafasi za kazi
447 na tangazo lingine lipo kwa lugha ya Kiswahili ambalo lina jumla ya
nafasi za kazi 877.
Aidha,
alizitataja baadhi ya nafasi hizo za kazi zilizoko katika tangazo la
kazi kwa lugha ya Kiswahili kuwa ni Mhandisi kilimo (agro–engineers),
Afisa kilimo (agro–officers) Mkufunzi kilimo (aquaculture), Afisa kilimo
msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary
officers), Daktari utafiti mifugo (veterinary research officer), Daktari
mifugo mkufunzi (veterinary tutor), Mkufunzi mifugo (animal science),
Afisa mifugo (live stock officer), Afisa utafiti mifugo (livestock
research officer), Afisa Utumishi (human resources officer), Afisa ardhi
msaidizi, Dereva (driver).
Nafasi
nyingine ni pamoja na Afisa utalii, Afisa ushirika (cooperative
officer), Afisa Serikali za mitaa (local government officer) Mhandisi
ufundi (mechanical engineer), Mhandisi haidrojiolojia (hydrogeologists),
Mhandisi (maji) – water resource engineer, Mhandisi (maji) – water
resource with gis engineer, Mhandisi (umeme) Mhandisi mazingira
(environmental engineer), Mhandisi kilimo (agro – engineers), Afisa
kilimo (agro – officers), Mkufunzi kilimo (aquaculture), Afisa kilimo
msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary
officers), Daktari utafiti mifugo (veterinary research officer).
Kada
nyingine ni Daktari mifugo mkufunzi (veterinary tutor), Mkufunzi mifugo
(animal science), Afisa mifugo (live stock officer), Afisa utafiti
mifugo (livestock research officer), Afisa ardhi msaidizi, Afisa utalii,
Afisa ushirika (cooperative officer), Ufundi (technician mechanics),
Fundi sanifu - ufundi (technician mechanics), Fundi sanifu - umeme
(technician electrical), Fundi sanifu – (water works technician), Fundi
sanifu maabara– (water laboratory technician), Fundi sanifu - maji -
(technician- water),Fundi sanifu msaidizi (ufundi bomba) - (assistant
water works technician plumbing).
Wengine ni
Fundi sanifu msaidizi (upimaji ardhi) - (assistant water works
technician geometric), Fundi sanifu msaidizi mitambo ya maji
(pampu),Fundi sanifu msaidizi mitambo ya maji (umeme), fundi sanifu
msaidizi - (assistant technician welding), Mhandisi - ujenzi (engineer–
civil), Fundi sanifu – ramani (technician - (mapping) na Mpiga chapa
msaidizi (assistant printer) .
Kwa upande
wa Tangazo la Kingereza kazi zilizotangazwa ni pamoja na "Senior
research engineer", "Research engineer assistant", "Principal engineer",
"Engineer", "Artisan", "Chief accountant", "Human resource development
and administrative manager", "Human resource development and
administrative officer", "Welder", "Tutor", "Principal planning and
promotion officer", "Director of planning, finance and administration",
"Tutors (travel & tourism), "Supplies officer", "Mediator",
"Arbitrator", "State attorney", "Personal secretary"," Office
assistant", "Security guard", "Receptionist", "Transport officer", "Law
secretary", "Computer system analyst", "Librarian assistants",
"Procurement specialist", "Director of nutrition policy and planning",
"Assistant medical officer", "Director of finance and administration",
"Environmental management officer-science".
Daudi
alifafanua kuwa nafasi hizo za kazi zilizo kwenye katika tangazo la
lugha ya Kiswahili ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Shinyanga, Dodoma,
Kilimanjaro, Dar es Salaam na Rukwa, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Morogoro, Sikonge, Liwale, Handeni, Iramba, Sumbawanga,Iringa,
Tanga, Ileje, Korogwe pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aliongeza
kuwa kwa tangazo la kazi la lugha ya Kiingereza waajiri wake ni pamoja
na Mamlaka na Bodi zifuatazo;- Tanzania Engineering and Manufacturing
Design Organization (TEMDO), Tanzania Automotive Technology Centre
(TATC), Ardhi Institute Morogoro, Tea Board of Tanzania (TBT), National
College of Tourism (NCT), The Commission for Mediation and Arbitration
(CMA), Attorney General’s Chambers, Tanzania Food and Nutrition Centre
(TFNC), Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), The National
Environment Management council (NEMC) and The Cashewnut Board of
Tanzania.
Katibu
amesema Utumishi wa Umma unahitaji watu makini, wenye weledi katika
taaluma zao na wenye maadili mema, kwa kuwa mtumishi wa umma ni kioo cha
jamii anaetakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuiwezesha Serikali
kutimiza malengo yake kwa ufanisi, ndio sababu ofisi yake inasisitiza
waombaji wa kazi kujiandaa vizuri ili kuweza kushindana na wengine wenye
uwezo kama wao. Hivyo, amewataka waombaji wa nafasi za kazi kutembelea
wao wenyewe tovuti hiyo ya Sekretarieti ya Ajira ili kujua nafasi na
daraja la kazi lililotangazwa ili kuepuka uwezekano wa kupewa taarifa za
kupotoshwa na kuomba kazi ambayo haijatangazwa na kujikuta mwombaji
akipoteza fursa ya ajira bila ya sababu za msingi.
Mwisho
amebainisha kuwa mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi hizo
zilizotangazwa ni tarehe 14 Julai, 2014 na kuwataka waombaji wote
kuwasilisha maombi ya kazi kwa njia ya posta kwa kutumia anwani
iliyowekwa katika matangazo ya kazi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
30 Julai, 2014.
0 comments: