ANGALIA PICHA MATESO ANAYOPATA MTOTO HUYU,MSAADA WAKO UNAHITAJIKA
Mtoto Hussein Jumbe mwenye umri wa miaka 6 sasa.
HUSSEIN Jumbe
ni mtoto mwenye miaka 6 sasa, lakini hakui, kwani hajaweza kukaa wala
kuongea, mwonekano wake ni sawa na mtoto wa mwaka mmoja, imekuwa
kilio na majonzi kwa mama yake mzazi, Rukia Twalibu, mkazi wa Kilwa
–Masoko, Mkoa wa LindiAkizungumza
kwa masikitiko makubwa na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Rukia alisema alimzaa Hussein mwaka
2008 huko Kilwa lakini katika kukua imekuwa ni tatizo kubwa ambalo
linaambatana na kushindwa kuongea wala kukaa. “Hapa
unapomuona anasikia kila kitu, anajua kila unachomuuliza lakini hawezi
kukaa wala kuongea. Muda mrefu nampakata au analala tu,” alisema
mwanamke huyo.
Mtoto Hussein Jumbe akiwa na mama yake mzazi, Rukia Twalibu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Alisema
baada ya mwanaye huyo kufikisha miaka miwili, baba yake mzazi alitoweka
katika mazingira ya kutatanisha hadi sasa hajulikani alipo kitu
ambacho kimempa wakati mgumu sana.
Akaendelea: “Nilipobaini hali
hii ya mtoto na sina msaada, nilikwenda Hospitali ya CCBRT (jijini Dar)
lakini madaktari wa hospitali hiyo walisema ukubwa wa tatizo la
mwanangu hawawezi kufanya chochote.
“Juni 22, mwaka huu ndiyo
nilikuja hapa Muhimbili ambapo mwanangu anachunguzwa kisa cha kutokua
kama watoto wengine ilhali umri unakwenda, bado madaktari hawajaniambia
chochote, naamini wanaumiza kichwa kujua tatizo.
Bi. Rukia akijaribu kumkalisha mwanaye.
“Hadi
kufika hapa Muhimbili nimepata michango kwa watu pia nilipata barua
kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi ambayo ilinisaidia kupata
kiasi kadhaa cha pesa,” alisema mama huyo.
Rukia
na mwanaye amelazwa katika Wodi ‘A’ ya Watoto, kwa aliyeguswa na
tatizo la mtoto Hussein, awasiliane na mama yake kwa namba 0714 177
071.
0 comments: