UKATILI BINTI WA BADARA LA SABA ABAKWA NA WANAUME WATATU
Mwanafunzi wa kike wa darasa la saba anayesoma katika Shule ya Msingi Chanzige B iliyopo Kisarawe, Pwani aliyefanyiwa unyama wa kulawitiwa na vijana watatu.
Denti mmoja wa kike wa darasa la saba anayesoma katika Shule ya Msingi Chanzige B iliyopo Kisarawe, Pwani amejikuta katika wakati mgumu baada ya kulawitiwa na kusababishiwa maumivu makali sehemu zake za siri.
Simulizi
ya binti huyo inayouma sana, inaeleza kuwa denti huyo alifanyiwa unyama
huo na vijana watatu ambao bado hawajafahamika majina yao mara moja
lakini amekuwa akimtaja mmoja kwa jina la Musa.
Tukio
hilo lenye sura ya majonzi hasa kwa wazazi na watoto, lilitokea hivi
karibuni Kisarawe mkoani Pwani lakini ilifanywa siri kwa muda mrefu na
mtoto huyo kukaa bila matibabu.
Chanzo
chetu cha habari kinasema kuwa, shangazi wa mtoto huyo ambaye anaishi
naye ndiye sababu ya kutopata tiba, kwani anadaiwa kuchukua kiasi cha
shilingi 200,000 kutoka Musa anayetajwa kuwa mmoja wa wahusika kama
kifunga mdomo.
Chanzo
hicho kikazidi kusema kuwa, awali kesi hiyo ilifikishwa katika Kituo
cha Polisi Kisarawe na kufunguliwa jalada lakini shangazi wa mtoto huyo
aliamua kuyamaliza mambo hayo na mmoja wa watuhumiwa baada ya kupewa
kiasi hicho cha fedha.
Uchunguzi
wa Amani umegundua kuwa, sakata hilo liliripotiwa katika Kituo cha
Polisi Kisarawe na kufunguliwa jalada nambari KIS/RB/326/2014, ambapo
Fomu ya Polisi Nambari 3 (PF3) ilitolewa kwa ajili ya matibabu ya mtoto
huyo.
Akisimulia
zaidi, mama mzazi wa mwanafunzi aitwaye Mariam Said alisema, alipata
taarifa za mwanaye kukumbwa na masahibu hayo ambapo aliamua kusafiri
kutoka Mlandizi anapoishi hadi Kisarawe kufuatilia tukio hilo.
Binti
huyo alisema alifanyiwa ukatili huo wakati akitokea shuleni na kwamba
alimweleza shangazi yake kila kitu kuhusiana na tukio hilo kabla ya
kwenda naye polisi kutoa taarifa.
“Baada
ya hapo tulikwenda katika Hospitali ya Kisarawe lakini sikupata
matibabu kwa sababu shangazi alisema hana pesa ya malipo, kukarudi
nyumbani na kununua dawa kwenye maduka ya dawa,’’ alisema mtoto huyo na
kuongeza:
“Pale
hospitalini, shangazi alitakiwa kutoa kadi ya Bima au shilingi 10,000
ili nitibiwe. Sasa hakuwa na Bima wala hiyo pesa ndiyo maana
ikashindikana.”
Gazeti
hili lilifunga safari hadi Shule ya Msingi Chanzige B na kuzungumza na
Mwalimu Mkuu, Issac Eliah ambaye alikiri kupokea taarifa ya mwanafunzi
wake kubakwa na kulawitiwa kutoka kwa shangazi wa mtoto huyo na kutoa
ruhusa kwa ajili ya matibabu.
Shangazi
wa mtoto huyo alipotakiwa kuzungumzia ishu ya kuzima kesi hiyo kwa
madai ya kupewa shilingi 200,000 alisema: “Mimi sitaki kuzungumzia suala
hilo, nendeni polisi mkaulize siyo kuniuliza mimi.”
0 comments: