ANGALIA PICHA MZEE WA KANISA AAIBIKA
Tumekwisha!
Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa
jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya
kukurupushwa kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka
kuvunja amri ya sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za
Kibongo, Debora Jacob, Ijumaa lina kisanga cha aina yake.
HABARI KAMILI
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi
kulisahahu maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na
Kituo Kikuu cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee
huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya
miaka 18.
.....akitaitiwa.
TUHUMA NZITO
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya
Global Publishers, ikiwa kwenye mingo zake, ilipokea simu kutoka kwa
dada aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana na kujieleza kuwa anatoka
kundi la sanaa za maigizo la Vivif lililopo Segerea jijini Dar.
OFM: Ndiyo hujakosea unazungumza na
OFM, tukusaidie nini?
Diana: Kuna mzee wa kanisa la kiroho la
(anataja jina la kanisa hilo) lililopo maeneo ya Segerea, aliomba kuwa
mfadhili wa kundi letu.
Tulimkubalia na baada ya muda alianza kutumia fedha zake vibaya kwa kufanya vitendo visivyofaa.
OFM: Vitendo gani visivyofaa?
Diana: Anawarubuni mabinti wadogo anawaweka kambini na kula nao tunda tamtam eti ndiyo tiketi ya kuchezeshwa kwenye maigizo.
OFM: Tiririka!
Diana: Yaani hadi muda huu ninapozungumza
na ninyi mzee huyo wa kanisa anachati na msanii mwingine wa kundi hilo.
Anaitwa Debora anataka waende kwenye gesti fulani wakanogeshane, wahini
tayari mtego umewekwa utafyatuka muda wowote.
UDHALILISHWAJI?
Diana alisema baada ya Debora kuombwa
‘mambo’ ndipo akawataarifu wasanii wenzake na kuwataka wote kwa pamoja
waungane kuikomesha tabia hiyo chafu ya Luca anayelichafua kanisa la
kiroho na kulidhalilisha kundi lao la sanaa.
OFM MZIGONI
Baada ya kuseti kila kitu, Diana aliiomba
OFM iambatane nao kwani muda huo tayari Debora alishatangulia kwenye
gesti hiyo kumfuata mzee huyo wa kanisa ambaye alishachukua chumba.
Taarifa hiyo ilipokelewa kwa mikono miwili
na kiongozi wa OFM ambaye aliwaagiza vijana wake makini ambao
walisitisha kazi nyingine za kiintelijensia kisha kuelekeza nguvu zao
eneo la tukio.
Vijana hao walitumia pikipiki zao ziendazo
kasi ambapo baada ya muda usiozidi dakika ishirini walikuwa wamefika
kwenye gesti hiyo.
ENEO LA TUKIO
OFM walipofika eneo la tukio, walikuta
kundi la wasanii hao wakimchomoa gesti mzee huyo wa kanisa ambaye
aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya viazi.
Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi
la wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye
chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya
wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa
wao la sivyo wangeichoma moto.
Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku
akihatarisha maisha yake kwa kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona
yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye
kanisani.
KABANG!
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa
aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili
akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.
APELEKWA MSOBEMSOBE KANISANI
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka kanisani
msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti
wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa
wakati akipelekwa kanisani.
MTAANI WERAAA!
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa
wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa
madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.
Wakiwa kanisani hapo polisi
walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na waumini wa kanisa
hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
BREKI YA KWANZA POLISI
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa
hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi
hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha
kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo
alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO,
KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18
NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.
Hadi OFM wanaanua jamvi kituoni hapo kanisa lilikuwa likihaha kumchomoa kwa dhamana akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
GPL
0 comments: