MKUTANO WA 64 WA FIFA WAFUNGULIWA SAO PAULO, BLATTER NA WAZIRI WA MICHEZO BRAZIL WAUNGURUMA
Mwimbaji wa Brazil, Maria Rita (kushoto, mbele), mwanamitindo Fernanda Lima (kulia, mbele ) wakitumbuiza katika mkutano huo.
SAO PAULO, Brazil
Rais wa shirikisho la soka duniani, FIFA, Sepp Blatter amefungua mkutano wa 64 wa shirikisho hilo, mjini Sao Paulo jana jioni.
Maofisa wa juu wa FIFA, mashirikisho sita wanachama wa FIFA na wanachama 206 vya vyama walihudhuria mkutano huo.
Blatter
pamoja na Wazili wa michezo wa Brazil, Aldo Rebelo walitoa hotuba zao
kwenye mkutano huo wakizungumzia fainali zinazoanza kesho nchini Brazil.
Mkutano
huo uliambatana na zawadi mbalimbali, burudani kutoka kwa wasanii na
mambo yaliiva zaidi pale mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa mwenye miaka
80 kwa sasa, Just Fontaine alipozawadiwa kiatu cha Adidas chenye madini
ya almasi.
Nyota
huyo alifunga mabao 13 katika mechi sita za kombe la dunia
lililofanyika nchini Sweden mwaka 1958 na kuiongoiza Ufaransa kushika
nafasi ya tatu, huku akiibuka mfungaji bora wa pekee katika historia ya
fainali za kombe la dunia. Rekodi yake haijavunjwa mpaka leo.
Kwa
kuwa fainali za 1958 hazikuwa na zawadi ya kiatu cha dhahabu, Fontaine
alisema jana usiku kuwa kiatu hicho ni zawadi maalum kwa mke wake na
timu yake ya Ufaransa.
Muda
wa jioni, wawakilishi mbalimbali, Josephine King (OFC), Hassan Shehata
(CAF), Mirabror Usmanov (AFC), Jozef Venglos (UEFA), Maria Coto
(CONCACAF), Carlos Valderrama (CONMEBOL) na Antonio Mattarese
(FIFA)walipata nafasi kuzungumza machache.
Kabla
ya kufungua mkutano huo, kamati ya utendaji ya FIFA ilikaa kikao mjini
Sao Paulo na kuwahakikishia Brazil kuwa watapa msaada kamili kutoka
shirikisho hilo na wana imani nao kwa uwezo mkubwa walioonesha kuandaa
kombe la dunia linaloanza kutimua vumbi kesho mjini Sao Paulo.
Pia Kamati ya utendaji katika mkutano huo iliwasilisha kanuni 10 za mpira wa miguu wa wanawake ikihitaji zipitishwe.
Mshambuliaji wa zamani wa Brazil, Edson Arantes do Nacimento "Pele" akijibu maswali mjini Sao Paulo
Kuhusu
kashfa za rushwa wakati wa upigaji kura ya kumpata mwenyeji wa fainali
za kombe la dunia kwa mwaka 2022, kamati ya utendaji ilisema suala hilo
liachwe katika kamati ya maadili ili imalize kazi yake kabla ya kutoa
msimamo wake.
Pia
mkutano huo ulibariki maamuzi ya kuzisaidia Bosnia na Herzegovina,
Croatia, Romania na Serbia msaada wa dola za kimarekani milioni mbili
ili kuimarisha miundombinu ya soka ambayo iliharibiwa na mafuriko
makubwa siku za karibuni.
Pia
kamati ilithibitisha kuwa Mexico itaibadili Canada katika fainali za
Olympik za soka la vijana la wanawake zinazotarajia kufanyika China
mwaka huu.
Mkutano huo wa FIFA unamalizika leo jioni.
0 comments: