SHAMBULIO JINGINE TENA LATOKEA KENYA LAUA 10
Shambulizi
lengine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu , pwani ya
Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.Shambulizi la leo limetokea siku
moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyowaua watu
50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha.
Kundi
la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia shirika la
habari la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini
Kenya.
Takriban
watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia
Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi
pamoja na kuteketeza magari.
BBC
0 comments: