WAASI 100 WALIOUAWA LEO SUDAN NDANI YA MASAA 3
Msemaji
wa jeshi Sawarmi Khaled Saad anasema kuwa mauaji hayo yalifanyika
wakati wa mapigano yaliyodumu muda wa saa tatu ya kuzima shambulizi eneo
la El Atmor.
Waasi
kutoka kwa kundi la (Sudanes Peoples Liberation Movement North)
walithibitisha shambulizi hilo na kusema kuwa ni wapiganaji watatu tu
waliouawa.
Kundi hilo limekuwa likiipiga vita serikali ya Khartoum eneo hilo kwa kipindi cha miaka 20 sasa
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na vita nchini humo.
Vita
hivyo vimezuka wakati Rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wa
Sudan Kusini wakitarajiwa kukutana leo kwa mazunguzmo ya amani , ukiwa
mkutano wa kwanza katika kipindi cha mwezi mmoja na wa pili tangu vita
kuzuka nchini Sudan Kusini.
Mazungumzo ya kwanza kujaribu kuleta amani kati ya pande zinazohasimiana yamecheleweshwa kwa zaidi ya mara maoja.
Wajumbe
kutoka pande zote wamekuwa wakikutana katika hoteli za kifahari nchini
Ethiopia tangu mwezi Januari ingawa hakuna hatua zozote zimefikiwa za
suluhu ya kudumu huku pande zote daima zikijadili kuhusu swala tete la
ajenda.
Mkataba
wa kusitisha vita uliotiwa saini na Kiir na Machar tarehe 9 mwezi
Mei,umekuwa ukikiukwa na kuvunjwa na pande zinazozozana kwenye mgogoro
huo ambao tayari umesababisha vifo vya maelfu na kuwalazimisha wengine
milioni moja nukta tatu kutoroka makwao.
Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Tedros Adhanom amesema kuwa pande zote husika kwenye mgogoro huo zimetenda uhalifu wa kivita.
0 comments: