MASTAA BONGO MUVI WAMLILIA RECHO
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akilia kwa uchungu.
MASTAA
wa Bongo Muvi wamemlilia msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho'
aliyefariki jana saa mbili usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
jijini Dar baada ya kujifungua ambapo mtoto wake alifariki muda mfupi na
baadaye yeye akafariki.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel
utasafirishwa kwenda kwao Songea kwa ajili ya maziko. Habari nyingine
za msiba zitatolewa wakati wowote na mtandao huu mara tu zinapopatikana.
(Stori: Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha/GPL)
0 comments: