SUAREZ AWAPIGA `CHANGA LA MACHO` REAL MADRID, BARCELONA, ASEMA YEYE `NGADO KWA NGADO` NA LIVERPOOL YAKE



Imechapishwa Mei 27, 2014, saa 9:34 asubuhi
LUIS
Suarez amemwambia mchezaji mwenzake wa Liverpool kuwa ana mpango wa
kubakia klabuni hapo msimu ujao ili kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa
wa ligi kuu soka nchini England.
Jana
jumatatu, Liverpool walisema kuwa kocha mkuu Brendan Rodgers amesaini
mkataba mpya utakaomuweka Anfield mpaka mwaka 2018 na atapata nguvu
zaidi kwa uwepo wa Suarez.
Ripoti
zinasema Real Madrid wameweka dau la paundi milioni 100 kwa ajili ya
kuinasa saini ya Suarez ambaye alisaini mkataba mrefu na Liverpool mwezi
desemba mwaka jana na aliahidi kukaa muda mrefu klabuni hapo.
Lakini
vyanzo vya habari Bernabeu vinaeleza kuwa hakutakuwa na haja ya
kumsajili Suarez kama Karim Benzema atakubali kusaini mkataba mpya.
Mfaransa
huyo ambaye yuko kwenye rada za Arsenal anahitaji kuongezewa dau na
Real Madrid, lakini klabu hiyo inaamini watafikia makubaliano na nyota
huyo mwenye miaka 26 kabla ya kombe la dunia.
0 comments: