WATANZANIA WANNE WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA JOMO KENYATTA
Watanzania
wanne (mwanaume mmoja na wanawake watatu) wamekamatwa na kilo 2.2 za
heroin kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Watanzania hao waliingia nchini Kenya kupitia Namanga na walikuwa njiani
kuelekea Hong Kong.
"Tumewakamata Watanzania wanne
leo (jana) JKIA. Tumewaweka chini ya uangalizi na tayari wameshatoa
vidonge 186 ambavyo tumevifanyia uchunguzi na kudhibitisha kuwa ni
heroin," Ngisa aliliambia Shirika la Habari la Uchina kwa simu.
Ameongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani leo Ijumaa.
na mdodosoaji
0 comments: