WATANZANIA WAHIMIZWA KUSOMA MAJARIDA MBALIMBALI ILI KUJIONGEZEA UFAHAMU
Cosmas Njingo-afisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro akichangia mada.
Zadock Kitomary-Mkulima bora mara mbili mfululizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha akitoa mada.
Ayubu Nnko-Msimamizi wa Jarida kwa upande wa Tanzania akitoa mada katika Semina hiyo. Coroline Nyakundi- Meneja Mradi The Organic Farmer& jarida la Mkulima mbunifu akitoa mada.
John Cheburet-Mtayarishaji wa vipindi vya Redio kutoka jarida la Mkulima mbunifu .
******
Ayubu Nnko-Msimamizi wa Jarida kwa upande wa Tanzania akitoa mada katika Semina hiyo. Coroline Nyakundi- Meneja Mradi The Organic Farmer& jarida la Mkulima mbunifu akitoa mada.
John Cheburet-Mtayarishaji wa vipindi vya Redio kutoka jarida la Mkulima mbunifu .
Na Arusha yetu Blog
IMEELEZWA kuwa Watanzania ni wavivu wa kusoma Majarida mbali mbali yanayoweza kuwaongezea upeo ukilinganisha na nchi zingine.
Hayo
yamebainishwa na Mmoja wa maafisa wa Jarida la Mkulima Mbunifu,
Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, wakati akizungumza katika mafunzo
ya waandishi wa habari za kilimo na wataalamu wa kilimo yanayofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Arusha Crown ya Mjini hapa.
Ameongeza
kuwa kunatofauti kubwa ya Mwitikio wa kusoma machapisho kati ya Raia wa
Tanzania ukilinganisha na Kenya ambako imeelezwa kuwa wanauhitaji
mkubwa wa kujifunza mbinu mpya za kilimo tofauti na Watanzania ambao
hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua zaidi.
Akieleza
Mikakati ya Jarida la Mkulima Mbunifu mmoja katika ya Maafisa wa Jarida
hilo, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya, amesema tangu kuzinduliwa
kwa jarida hilo Juni,2011 limeonesha mwitikio mkubwa kutokana na kupata
taarifa nyingi kutoka kwa wakulima wakilihitaji ili kujua zaidi habari
za Kilimo.
Amesema
Jarida hilo limelenga zaidi maoni na mahitaji ya Mkulima kutokana na
mawazo yao ambayo wamekuwa wakiyatoa katika jarida hilo mara kwa mara
jambo linaloonesha Mkulima kufikiwa na Jarida hilo na kwa wakati.
0 comments: