RAISI KIKWETE AHUSISHWA UTAPELI , IKULU YATOA ONYOO KALI

WAKATI Kukiwa na utitiri wa kundi la matapeli kwa njia ya mitandao unaoendelea kutokea kila siku matapeli hao wameanza kutumia jina la Rais Jakaya Kikwete,Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mtoto wa Rais Kikwete  Zainab Kikwete pamoja na jina la Rais wa Marekani Barack Obama. Haya ni majina makubwa nchini ambayo yakitumika katika suala lolote nchini ni rahisi kwa wananchi kuamini na kuamua kujitosa katika mchakato wowote hususan michakato ya kifedha na maendeleo.
Rais Jakaya Kikwete akifafanua jamboTaasisi hiyo inayoitwa Tanzania Loans Society ambayo inajitangaza kwamba ni tawi zawa la Shirika kubwa nchini marekani liitwalo Advolticies Power Loans Society (APL Society) linalo'ongozwa na Rais Barack Obama imekuwa ikitapeli wananchi.
Taarifa zao zinasema kwamba Tanzania Loans Society ni tawi ambalo limeanzishwa mwaka 2012 kwa dhumuni la kutaka kuwasaidia watanzania ambao wanahali duni (masikini) kwa kumuwezesha kumpatia kila mtanzania mkopo wa fedha mikopo inatolewa kwa kila mtanzania atakaejiunga na kua mwanachama wa Tawi hili.
Sehemu ya Maelezo ya taarifa za taasisi hiyo ilifafanua kuwa "Tawi hili lilianzishwa nchini Tanzania baada ya Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania alipokua katika ziara yake nchini marekani alipata fursa ya kuonana na Rais Barack Obama".
Taafira inaeleza kwamba Rais Kikwete alipewa muongozo na mchanganuo wa shirika la kuwasaidia wamarekani (APL Society) wasiokua na uwezo wa kifedha. Rais Barack Obama alikua na moyo thabit wa kuonesha kujali na akawa tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete dhidi ya wananchi wake masikini akamshauri kikwete afungue tawi dogo ambalo litakua ni sehemu moja wapo ya shirika la APL SOCIETY ili kuwasaidia watanzania kupata fedha za mikopo".
Taarifa zaidi zinasema kwamba "Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho kikwete alikubaliana na shauri hilo la Rais Barack Obama na kukubali kuanzisha tawi zawa la APL Society na kulipa jina Tanzania Loans Society, Rais Kikwete alitia saini ya makubaliano ya wazi nchini marekani na zilitolewa fedha za mtaji wa kuanzishwa kwa tawi hili na jumuia ya madola nchini marekani kiasi cha shilingi billion miatano".
Lakini kutokana na majukumu ya Rais jakaya mrisho kikwete kuwa mengi hivyo ikawa ni vigumu kwa yeye kusimamia na kuendesha mradi huu hivyo aliamua kugawa majukumu haya kwa Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo pamoja na Zainabu Kikwete ambae ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Bank kuu ya Tanzania (B.O.T) na NMB.
Rais Jakaya Kikwete (kulia),akisalimiana na Rais Barack Obama, alipomtembelea katika Ikulu ya Marekani White House.Tanzania Loans Society inawakilishwa na Rais Jakaya kikwete, inaongozwa na General Manager Mh. Mizengo Pinda na inamilikiwa na Loan Officer Zainab Kikwete kwa udhamini wa Rais Barack Obama. Lengo la kuanzishwa Tanzania Loans Society ni kutaka kuwasaidia watanzania wenye hali ya chini kimaisha
Nifursa kwa kila mtanzania mwenye umri wa miaka kuanzia 18 na mwenye akili timamu ajiunge na chama cha Tanzania Loans Society ili aweze kupata msaada wa kifedha.
Tutahakikisha kila mtanzania atakaejiunga na chama hiki kwa kujaza fomu ya uanachama na akachangia ada ya uanachama Tshs. 83,000 akawa mwanachama wa Tanzania Loans Society atapatiwa mkopo wa fedha anaohitaji pia kila atakaejiunga tutampatia mkopo wa pesa.
Mtu yoyote anaruhusiwa kujiunga na mradi huu ili kutimiza ndoto zake unachotakiwa nikua na vigezo vifuatavyo, uwe ni mtanzania, uwe na akili timamu, uwe umetimiza miaka18 na uwe na kitambulisho cha aina yoyote ile.
Kama unavigezo tajwa hapo unaruhusiwa kujaza fomu na ukajiunga ukawa mwanachama na kuchukua mkopo wa fedha kiasi chochote unachohitaji kuanzia laki moja na kuendelea, kila atakaejiunga nakua mwanachama wetu tutampatia zawadi ya shilingi laki tatu bure.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika moja ya vikao vya Bunge mjini Dodoma.Kuhusu UTARATIBU WA KUJIUNGA: "Kujiunga na ili uwe mwanachama ni Rahisi Sana unachotakiwa ni kujaza fomu iliyopo Online katika tovuti hii utaiona Link hapo chini ya kujaza fomu imeandikwa "JAZA FOMU HAPA" katika fomu hii kuna sehemu utajaza kiasi cha fedha unachotaka ukopeshwe Ukishajaza fomu yote utatakiwa kuchangia mfuko wa wanachama kwa kulipia ada kama udhamini wako wa uanachama kiasi cha Tshs. 83,000 (elfu themanini na tatu).
Taarifa za taasisi hiyo iliyotajwa kuwa ni ya kitapeli na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu iliongeza kuwa "Baada ya kujaza fomu na kulipia ada ya Uanachama elfu thelathini na tisa kwa njia ya M-Pesa katika namba ya M-Pesa pesa itapokelewa na Loan Bord Officer wa Tanzania Loans Society ambae pia ni muweka hadhina wa bank kuu ya Tanzania BOT "Zainab KIKWETE"
"Namba ya kulipia ada ni 0716 745 387 jina litatokea Zainabu KIKWETE wakati wa kutuma pesa pia unaweza ukatuma kutoka tigo kuja voda au voda kwa voda. ukishalipia utatumiwa Code namba yako ya Uanachama na ndani ya dakika30 utatumiwa kiasi cha fedha za mkopo ulizohitaji"
Kuhusu MAREJESHO YA MKOPO: Marejesho ya mkopo yataanza kufanyika baada ya miezi miwili kupita kuanzia siku uliyochukua mkopo, utakapopatiwa mkopo utatakiwa ukae miezi miwili bila kulipia na baada ya hapo utaanza kua unalipia kila mwezi Tshs. 60,000 (elfu stini) mpaka deni lako lote litakapokwisha na hakuna riba kwa sheria ya dini hivyo utakachokopa ndicho utakacholipa.
JINSI YA KUJIUNGA UPATE MKOPO: Kujiunga ni rahisi sana bofya katika hiyo link ifuatayo hapo chini imeandikwa "JAZA FOMU HAPA" Utaikuta fomu ya kujiunga ijaze kisha lipia ada Tshs.83,000 utapatiwa mkopo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu(kushoto),katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali Assah Mwambene.Picha zote na Maktaba ya Habarimpya.comJAZA FOMU HAPA:Ada ya Uanachama pamoja na Marejesho ya Mkopo vitalipiwa kwa njia ya Technolojia ya Mobile banking kwa udhamini mkuu wa VodaCom ili kurahisisha huduma hii. Kwa wateja wa Vodacom M-PESA watalipia katika namba: 0716 745 387
MAREJESHO YA MIKOPO: Kila atakaepatiwa mkopo atatakiwa akae miezi miwili (wiki8) kisha baada ya hapo atatakiwa kuanza kufanya marejesho kila mwezi kwa kulipia kiasi cha Tshs. 60,000 (elfu stini) kila mwezi mpaka deni lake litakapokwisha.
Hata hivyo Habarimpya.com ilimtafuta Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali Assah Mwambene pamoja Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kupitia simu zao za mkononi lakini ziliita bila kupokelewa.

Hatimaye Habarimpya.com ikamtafuta Mkurugenzi wa Mawasiliano wa IkuluSalva Rweyemamu ambaye alisema kwamba hao ni matapeli na kwamba wananchi wanapaswa kuwa makini kwa utapeli unaozidi kukua katika sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mitandao ya kijamii. "Hao ni matapeli hivi kweli ninani anayeweza kukupa pesa kirahisi rahisi katika dunia ya leo, sisi tunashukuru kwa taarifa hii tutaifanyia kazi lakini jibu langu ni kwamba huo ni utapeli na wananchi wasikubali kurubuniwa"alisema Rweyemamu.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/