MAPENZI YANAVYO MTESA LOWASSA, KUMNYIMA URAIS
WAKATI Waziri Mkuu aliyejiuzuru
ambaye ni Mbunge wa Monduli Mkoani Arusha Edward Lowassa, pamoja na
makada wengine sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifungiwa kushiriki
katika matukio yoyote ya siasa ndani na nje ya nchi,imebainika kwamba
mapenzi ya siasa ndiyo yanayomtesa mbunge huyo.
Kichwa cha Lowassa kikiwa kwenye noti ya tsh 500Lowassa
anateswa na mapenzi kiasi cha kuwa kero kubwa hata kwa wapinzani wake
ambao kwa njia moja ama nyingine wamekuwa wakitafuta kila njia ya kuzika
nyota yake inayong'aa kila kukicha.
Mapenzi hayo ndiyo yalisababisha yeye na wenzake, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambaye ni Mbunge wa Bumbuli January Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, Waziri Mkuu Mstaafu Fredirick Sumaye pamoja na William Ngeleja kufungiwa kufanya siasa kwa sababu tu ya mahaba ya Lowassa. Moja ya Sababu iliyotajwa kuhusu Lowassa ni kwamba alikua akigawa pesa kwa nia ya kujiimarisha na kutafuta njia ya kukubalika kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Hatua hiyo iliwekewa mkazo mzito kufuatia suala la flana zilizokuwa na jumbe mbalimbali ikiwemo friends of Lowassa ambazo zilitengenezwa maalum na kutumika siku ya mwaka mpya ambapo aliita marafiki zake wote na kula nao pamoja. Hatua hiyo iliwachanganya wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho na kuanza kutafuta njia mbalimbali za kumkwamisha ingawa wamefanikiwa kwa namna moja ama nyingine ila mapenzi ya Lowassa bado yataendelea kumtesa yeye pamoja na Chama Chake Cha CCM.
Blogu ambayo imetengenezwa maalum kwa ajili ya kutangaza jina la Lowassa sehemu mbalimbali duniani.Mapenzi
yanayo mtesa Lowassa inatokana na wafuasi wake kuendelea kutafuta njia
mbalimbali za kueneza ujumbe unaonyesha kuwa anakubalika na kushawishi
wapiga kura wakubali kwamba anastahili kuwa Rais wa Tanzania.
Watanzania wanaomfanya Lowassa achanganyikiwe kwa mahaba hawana undugu wala hawafahamiani na Mbunge huyo wala hawatoki katika Jimbo la Monduli ila wamejikuta tu wakimpenda kutokana na umakini wake katika uongozi.
Mapenzi hayo yanazidi kumtesa Lowassa kiasi ambacho wamefikia hatua ya kuweka picha yake katika noti ya tsh 500 ikiwa ni ishara kwamba wanamapenzi na Mbunge huyo kama walivyo na mapenzi na pesa na kwamba picha yake inastahili kuwa katika pesa za Tanzania.
Makamu
Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela akionyesha moja ya fulana
ambazo amedai zimesambazwa nchi nzima, zikiwa na maneno Friends of
Lowassa ...Haya ndiyo mapenzi yanayomtesa Lowassa popote
alipo,nina imani kwamba Lowassa ni mtu makini mwadilifu na mvumilivu
mwenye hekma na busara, mwenye kuheshimu kila mtu na mtiifu mbele ya
Chama chake, hivyo angependa kutii amri ya CCM ya kukaa nje ya siasa kwa
kipindi cha mwaka mmoja bila jina lake kusikika wala kuzungumziwa kwa
njia yoyote ile.
Ila Lowassa anashindwa kutimiza sharti hilo kutokana na sumu ya mapenzi aliyoimwagwa kwa watanzania kwani pamoja na CCM kukataza shuguli za siasa kwa makada wake sita lakini kwa Lowassa hali hiyo imeoneka kugonga mwamba na pengine mahaba hayo ndiyo yatakayofanya CCM izidi kumchukia na kutengenezea mazingira magumu ya kutimiza ndoto zake kwani kila siku ataonekana mhaini na msaliti ingawa si yeye bali ni mapenzi yake kwa watanzania ambao kila kukicha wanabuni njia mbalimbali za kutangaza jina lake.

0 comments: