HUZUNI TELE...MWANAFUNZI NA MWENZAKE "MUOKOAJI" WAFA MAJI HUKO MKOANI SINGIDA...!SOMA ZAIDI HAPA...



Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ipembe mjini Singida, Rashid Said (16) (kushoto) na wa kijana ambaye hajafahamika jina aliyekuwa anajaribu kumwokoa mwanafunzi.
Mwili wa mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Rashid Said ambaye alikuwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ipembe, ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).

MWANAFUNZI Rashid Saidi (16) ambaye alikua kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Ipembe mjini hapa, amefariki dunia baada ya mtumbwi aliokuwa umeupanda ziwani, yeye na baadhi ya wanafunzi wenzake kupigwa na upepo mkali na kusababisha mtumbwi kupinduka na wao kutumbukia kwenye maji.

Kijana mmoja ambaye sio mwanafunzi na jina lake bado halijapatikana,alijitolea kumwokoa mwanafunzi huyo,lakini naye kwa bahati mbaya alifariki dunia baada ya kunywa maji mengi na kuzama ziwani.Tukio hilo la kusikitisha limetokea Machi nane mwaka huu saa nane mchana.

Inadaiwa kuwa wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha’tuition’ shuleni kwao,kama kawaida yao walienda ‘pikiniki’ katika ziwa la Kindai na kuanza kuogelea pembeni mwa ziwa hilo.

Askari kutoka kikosi cha zima moto mjini hapa,Bahati Hemed,amesema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na mashuhuda wa tukio hilo,ni kwamba baada ya wanafunzi hao kumwagwa ndani ya maji,baadhi ya wanafunzi walifanikiwa kujiokoa na Rashid ambaye hana uzoefu wa kuogelea,alizama ndani ya maji.

Amesema wanafunzi hao baada ya kutoka nje ya ziwa,walimwomba kijana mmoja ambaye alikuwa na umri mkubwa aingie ziwani ili akamwokoe mwanzao.

“Yule kijana aliyejitolea kumwokoa mwanafunzi, alipokaribia alikotumbukia mwanafunzi huyo, na yeye mambo yalimwendea vibaya na kusababaisha na yeye apoteze maisha” alisema Bahati kwa masikitiko.Alisema baada ya hapo waliweza kuita wavuvi ambao walifika na nyavu na kuweza kutoa miili hiyo miwili kutoka ndani ya ziwa Kindai.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/