JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LIMEWATIA MBARONI WATU NANE (8) KWA KUKUTWA NA KILO MOJA NA MISOKOTO 104 YA BANGI PAMOJA NA ZANA ZA KUVUNJIA USIKU YAKIWEMO MAPANGA, MKASI NA NONDO.
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia
watu nane (8) waliokamatwa wakiwa na kilo moja na misokoto 104 ya bangi, zana za kuvunjia yakiwemo
mapanga, mikasi, visu, nondo pamoja na mirungi gramu 500.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME - SACP amesema mafanikio haya yametokana na msako
unaoendelea Mkoani Dodoma wa kupambana na wahalifu na uhalifu
uliofanyika eneo
la Chang’ombe tarehe 11/03/2014 majira ya saa 01:00Hrs hadi 05:00Hrs na
ulihusisha zaidi kero za uvutaji wa bangi na kupelekea kufanya uhalifu
katika
maeneo mbalimbali manispaa ya Dodoma.
-SOMA HABARI KAMILI HAPAA>>http://http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/
JIUNGE NASI KWA FACEBOOK UPATE HABARI MOTOMOTO MDAU, HII HAPA >>>> www.facebook.com/pages/KIINI-CHA-Habari-kwetu-TZ/238209189679913
JIUNGE NASI KWA FACEBOOK UPATE HABARI MOTOMOTO MDAU, HII HAPA >>>> www.facebook.com/pages/KIINI-CHA-Habari-kwetu-TZ/238209189679913
Kamanda MISIME amewataja waliokamatwa katika msako huo kuwa ni:-
1. HALFANI S/O MUHEZA mwenye miaka 25,
Mgogo, Mkulima.
2. STEWART S/O SYLVESTER mwenye miaka
18, Mgogo, Mkulima.
3. SHABAN S/O IBRAHIM mwenye miaka 18,
Mgogo, Mkulima.
4. ABDALLAH S/O IDDI mwenye miaka 18,
Mnyaturu, Mkulima.
5. FIKIRI S/O JONAS mwenye miaka 20,
Mgogo Mkulima.
6. ALLY S/O NURU mwenye miaka 30,
Mgogo, Mkulima
7. SAIMON S/O ZABRON mwenye miaka 43,
Mchaga, Mkulima.
8. ALBERT S/O CHARLES mwenye miaka 18,
Mgogo, Mkulima wote wakazi wa eneo la Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
Watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani kesho tarehe 12/03/2014 kujibu tuhuma zao zinazowakabili.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
linaendelea kumtafuta Dereva wa gari linalosemekana kuwa ni TOYOTA LAND CRUISER
GX STANDARD rangi nyeupe baada ya kumgonga mpanda baiskeli aliyefahamika kwa
jina la JULIAS S/O SANDUKU mwenye miaka 50, Mkaguru, Mkulima, Mkazi wa Gairo
katika eneo la Kijiji cha Visimi Kibaigwa na kumsababishia kifo mpanda baiskeli
huyo.
Kamanda MISIME amesema dereva huyo ambaye alikuwa anatokea
Dodoma kuelekea uelekeo wa Mkoa jirani wa Morogoro baada ya kumgonga mpanda baiskeli huyo, alishuka
kutoka ndani ya gari na kumwangalia aliyemgonga alipogundua amefariki akageuza
gari kurudi njia ya Dodoma na kuwaambia wananchi waliojitokeza kuwa anaenda
kutoa taarifa Polisi jambo ambalo hakufanya.
Kamanda MISIME
amewaomba wananchi wenye taarifa na dereva huyo alipo wajulishe katika kituo
chochote cha Polisi ili aweze kukamatwa.

0 comments: