HIZI NDIZO TV ZITAKAZO ONYESHA MCHEZO BAINA YA YANGA NA AL AHLY
Kikosi cha Young Africans kilichowasili mchana wa jana jijni Alexandria kikitokea jijini Cairo kimefanya mazoezi katika uwanja huo utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa leo, huku morali ya wachezaji kuelekea mchezo huo ikiwa ni ya hali ya juu sana.
Wachezaji 20 waliopo Alexandria wamefanya mazoezi chini ya makocha Hans Van der Pluijm, Charles Mkwasa pamoja na kocha wa makipa Juma Pondamali anayewanoa magolikipa na kuhakikisha wanaendelea kuwa fit kwa ajili ya mchezo huo.

Kuelekea mchezo wa leo ambao utaonyesha na televison zaidi ya 8 za nchini Misri, maandalizi yote yameshakamlika na katika kikao cha maandalizi ya mechi kamisaa ameendelea kusisitiza kuwa mchezo hautakua na mashabiki wa aina yoyote.
Wachezaji waliopo nchini Misri na kufanya mazoezi ya mwisho leo jioni ni"
Magolikipa: All Mustafa "Barthez", Juma Kaseja, Deogratias Munish "Dida" Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Kelvin Yondani "Cotton", Nadir Haroub "Cannavaro" Viungo: Haruna Niyonzima, Saimon Msuva, Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Nizar Khalfani Washambuliaji: Mrisho Ngasa, Said Bahanuzi, Emmanuel Okwi, Hamis Kizza, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu
Mechi itachezwa kuanzia majira ya saa 1kamili kwa saa za Misri sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, na leo hii mapema wapenzi, wadau na wanachama wa Young Africans watapatiwa link ya kuweza kutazama mchezo huo moja kwa moja kwa kutumia internte. Mungu Ibariki Young Africans, Mungu Ibariki Tanzania
0 comments: