KIPIMO CHA DNA HUENDA KIKALETA DOSARI KATIKA NDOA MKOANI MBEYA, NI KUTOKANA NA 40% YA WATOTO WANAZALIWA NDANI YA NDOA SIO WA WANAUME HALALSI.
ASILIMIA
40 ya Wanaume waliopima vinasaba ili kubaini uhusiano wa kibaiolojia na
watoto wanaowalea, wamebainika kuwa watoto hao si wao licha ya kuzaliwa
na wake zao au wapenzi wao.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega, bado kuna tatizo la wanaume wengi kubebeshwa mzigo wa kuwalea watoto ambao si halali yao, licha ya kuaminishwa na wenzao wao kuwa ni damu yao.
Mtega, ametoa taarifa hiyo kwenye mahojiano na waandishi wa habari jijini Mbeya wakati wa Warsha ya siku Moja ya kuwaelimisha Wateja wa huduma za Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini pembezoni mwa warsha hiyo, wanaume wanaona ni bora kulea mtoto bila ya kupima DNA kwani hatua hiyo ni hatari kwa uimara wa ndoa zao.
Hata hivyo, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Robert Mayala, amesema vipimo hivyo vimesaidia kutatua kesi nyingi za kubaini uhusiano baina ya baba na mtoto.
Warsha hiyo imewahusisha Waingizaji, Mawakala, Wasafirishaji, Wauzaji na Watumiaji wa kemikali na wadau wengine wa sekta hiyo wakiwemo TRA, Jeshi la Polisi, Madaktari na Waandishi wa Habari
0 comments: