KIKWETE , AZINDUA RASMI MTAMBO MAALUM WA USIMAMIZI NA UHAKIKI WA MAWASILIANO YA SIMU
Mgeni Rasmi Kuwasili Mheshimiwa Dk. Jakaya
Mrisho kiwete , Rais wa Serikari ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizindua Rasmi Mtambo Maalum wa Usimamizi na
Uhakiki wa mawasiliano ya Simu kwa kukata utepe ambapo sherehe hizo
zilifanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya Mtambo wa Kuhakiki
Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System)
aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar
es salaam.
Kulia ni Waziri wa
Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Pro, Makame
Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dkt Fenella
Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za
Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014
katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete , Rais wa Serikari ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akiwa akiwa katika 'Laptop' kwa ajili ya kubofya
ili kuruhusu Rasmi mtambo huo kuanza kufanya kazi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma
akitoa Maelezo ya kina kwa Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho kiwete , Rais
wa Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jinsi Mtambo huo
unavyofanya kazi
Mheshimiwa
Dk. Jakaya Mrisho kiwete , Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
akizungumza Jambo wakati wa uzinduzi Rasmi wa Mtambo huo.
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA TANGA AKAMATWA PEMBA AKIWA NA MIHARADATI
Na Masanja Mabula, PEMBA — JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba,
linamshikilia mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mwanaisha Kiyaka
Ayoub (30) mkaazi wa Pande Tanga na Chake Chake kwa tuhuma za
kupatikana na mafurushi ya bangi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa niaba ya kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Mlenge Mohammed Mlenge, alisema mtuhumiwa alikamatwa jana majira ya saa 11:50 alfajiri baada ya kushuka kwenye mashua katika bandari ya Wete akitokea Tanga.
Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi la polisi.
Taarifa za kwamba kuna mtu anakuja na bangi tulizipokea mapema na kuweka mtego hapa bandarini Wete, kwa kweli haikuwa shida kumkata alisema.
Aidha alisema baada ya kufanya upekuzi kwenye begi lake walimkutana mafurushi 22 ya bangi.
Aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono falsafa ya polisi jamii ambayo
imekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na matendo ya uhalifu. Alisema polisi wanaendelea kukamilisha uchunguzi kabla ya kumfikisha mahakamani. --- via ZanziNews
>>..wavuti

0 comments: