UVUMILIVU NI SOMO LA MAISHA, UPO TAYARI KUJIFUNZA?
Kuna
mtu mmoja alishawahi kusema hivi, “Mwonekano wako ni halisi
unapojionyesha wakati wa mambo magumu, huwezi kuwa zaidi ya hivyo katika
utu wako”. Ukiendelea kuwahukumu watu wengine kutokana na tabia zao
huwezi ukaona kitu kizuri ndani yao. Badala ya kumwona mfanyakazi
mwenzako ni mtata, msumbufu, katili , hana utu, jaribu kumwona mtu huyo
kama mwema na anahitaji kueleweka. Tafuta kitu kizuri ndani yake na
uweze kwenda naye kwa hicho kizuri.
Ingawa
mambo kama hayo yamejengeka kwa muda mrefu kutOkana na wapi mtu huyo
alizaliwa, maisha gani amepitia na mambo gani yameikabili familia yake
akiwa mtoto, kama wazazi kupigana, kutoonyeshwa upendo kwa wazazi wake
mwenyewe hivyo kuathirika na vitu vingi.
Unapojaribu
kuchukuliana na udhaifu wa mtu mwingine na jinsi alivyo unahitaji
uvumilivu. Fikiria kwamba kuna mfanyakazi unataka abadiLike kutokana na
tabia zake, je yuko hapo kukufundisha nini? je wanakupa mwangaza gani na
wewe kujiona kwenye kioo? Mara nyingine ni watu ambao unatakiwa
kujifunza kutokana na jinsi walivyo na utagundua mambo mengi ambayo
ulikuwa huyajui hasa kuhusu wewe mwenyewe.
Mfano,
kama unasimamiwa na mtu ambaye ujuzi wake ni mdogo kuliko wa kwako,
somo ambalo linatakiwa kukaa akili mwako ni namna ya kuchukuliana naye
na uvumilivu. Badala ya kulalamika na kumwona hafai kumbuka tu ya kwamba
‘sisi sote hujitaidi kufanya kazi kwa namna tunavyoweza kwa wakati
fulani’. Kuna wakati mwingine ninapenda msemo huu ‘naomba uwe mvumilivu
kwangu, Mungu bado hajamalizana nami’ kwasababu wote hatujakamiliaka
tunahitaji kuendelea kujifunza kila wakati.
Wakati
tumekatishwa tamaa na watu wengine kazini kwetu ama kwenye taaluma
zetu, tunatakiwa kujifunza kwa kiasi, kumbuka ulikotoka, halafu jitazame
sasa na wapi unaelekea na unafanya nini kwa matatizo unayopata eneo la
kazi. Jifunze kuvumilia na kusamehe. Kama ni sababu ya kitaaluma
unatakiwa kujifunza ujuzi usiokuwa nao ili kujiboresha, kusaidia wengine
wasioweza kama wewe hapo kazini kwa kuwafundisha ili waweze kujifunza
na kuwa na mazingira mazuri ya kikazi hapo.
Somo
la maisha ni zaidi ya masomo ya darasani, hivyo unatakiwa kujifunza
kila siku. Vyuo vyetu havina wanataaluma wanaosaidia kisaikolojia, wengi
wamekuwa wakitusaidia kufaulu masomo ya darasani na kwenye mahusiano.
Tunahitaji watu wanaoweza kusaidia fikra za watu kuondokana na mtizamo
hasi, uliojengwa na maisha ya mtu aliyopitia. Hutaweza kuwasaidia watu
wengine kazini kwako kama huna uvumilivu wa kuweza kuwasaidia wafanye
kinachotakiwa kufanyika.
0 comments: