PICHA ZINATISHA...UKATILI MKUBWA DAR...KIBAKA APOKEA KICHAPO KIKALI TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI...!!


 
Kutokana na hasira za watu hao walioamua kujichukulia sheria mkononi,sidhani kama alipona kwani baadaye walitokea mgambo wa jiji na kumuokoa, Wakati wakielekea katika kituo cha Polisi cha Karume Kibaka huyo alianguka na kupoteza fahamu kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi kichwani.
 


Mmoja wa wananchi mwenye hasira kali akimponda na tofari Kibaka ambaye jina lake halikujulikana mara moja baada ya kudaiwa kumkwapua abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari akisafiri kuelekea Mwenge akiwa ametokea Tandika.
 
Kibaka huyo inadaiwa alimkwapua simu abiria huyo na kukimbilia katika eneo la makaburi yaliyopo Karume na ndipo lilipoibuka kundi la Watu na kuanza kumfukuza na hatimaye kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshushia kibano cha nguvu kama uonavyo pichani.

RAIS KIKWETE AUNGANA NA JUMUIYA YA CHUO KIKUU KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA BALOZI KAZAURA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipowasili kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo Februari 27, 2014. Nyuma yake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe saidi Meck Sadick.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na waombolezaji wengine kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo Februari 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo Februari 27, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji familia ya marehemu kwenye hafla rasmi ya mazishi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Marehemu Balozi Fulgence Kazaura katika ukumbi wa Nkrumah Chuoni hapo leo Februari 27, 2014.

(PICHA NA IKULU)
- See more at: http://www.mdadisi.com/2014/02/rais-kikwete-aungana-na-jumuiya-ya-chuo.html#sthash.arTgGKwY.dpuf

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/