Argentina Yaichapa Switzerland na kutinga Robo Fainali
Hatua ya 16
bora ya michuano ya kombe la dunia inazidi kupamba moto – leo hii
Argentina walikuwa wanakipiga na Switzeland.Matokeo ya mchezo huo
Argentina wamefanikiwa kwenda hatua ya robo fainali kwa ushindi wa
1-0.Goli la dakika za nyongeza la kiungo mshambuliaji wa Real Madrid
Angel Di Maria lilihitimisha mchezo huo mgumu ambao mpaka kufika dakika
ya 90 milango yote ilikuwa migumu.
Argentina sasa anamsubiri mshindi wa mechi kati ya Belgium dhidi ya USA kwa ajili ya Robo fainali!
0 comments: