TAARIFA MPYA KUHUSU TAREHE YA KUWASILI KOCHA MAXIMO
Maandalizi
ya msimu wa ligi kuu ya Tanzania yameanza kupamba moto huku vilabu
vikijaribu kujiimarisha tayari kwa mapambano, kwa upande wa klabu ya
Yanga wameanza kwa kuimarisha benchi la ufundi kwa kumuajiri kocha
Marcio Maximo.Kocha huyo mbrazil anayeheshimika zaidi nchini, Marcio
Maximo atatua Jangwani ndani ya siku nne kuanzia leo Jumamosi. Bosi huyo
ambaye anasifika zaidi kwa msisitizo wake katika nidhamu za wachezaji
atatua Jumanne ikiwa ni mapema kabla ya uchaguzi wa Simba utakaofanyika
Juni 29 Jijini Dar es Salaam. Mwanaspoti linajua kwamba Maximo yuko
jijini Brasilia akifanya kazi ya uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia
kwenye televisheni ya Taifa ya Mexico na mkataba wake unamalizika
Jumatatu.
Yanga
imethibitisha kwamba Maximo ameshaanza maandalizi ya safari hiyo tangu
juzi ambapo katika hilo pia amewajulisha baadhi ya maofisa wa Ubalozi wa
nchi hiyo nchini kuwa atakuwa Tanzania mapema wiki hii kumalizia
maongezi yake na mabosi wa Yanga.
Yanga
wamemleta Maximo mapema kufanya maandalizi ya uhakika katika kikosi cha
timu hiyo ikiwa ni kuwawahi wapinzani wao wa jadi Simba ambao bado wapo
katika mchakato wa uchaguzi.
“Ilikuwa
kuna baadhi ya viongozi waende Brazil kumalizia mazungumzo na
kusainishana mkataba lakini hilo limebadilishwa. Maximo ndiyo atakuja
Dar es Salaam kuepuka gharama,”alisisitiza mmoja wa viongozi wa Yanga.
Source: Mwanaspot
0 comments: