MAREKANI YAIWEKEA UGANDA VIKWAZO KWA KUPITISHA SHERIA YA USHOGA
Marekani kuinyima Jeshi na Polisi wa Uganda ufadhili
Marekani
imeiwekea Uganda vikwazo kwa kupitisha sheria zinazopinga mapenzi ya
jinsi moja katika taifa hilo la Mashariki ya Afrika.
Afisa wa
mahusiano anayesimamia maswala ya usalama katika ikulu ya whitehouse
Caitlin Hayden anasema kupitia kwa barua kwa wanahabari kuwa sheria hiyo
iliyopitishwa na bunge la Uganda mwezi Februari inakiuka haki za
binadamu.
Vikwazo hivyo vitajumuishwa marufuku ya wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.
Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na ushirikiano na polisi wa Uganda Wizara ya Afya.
Sekta ya Afya na usalama wa taifa itaathirika na vikwazo hivyo.
Aidha
msaada kwa miradi iliyoanzishwa kwa usaidizi wa marekani pia utapunguzwa
mbali na kufutiliwa mbali kwa mazoezi ya kijeshi kati ya majeshi ya
uganda na yale ya Marekani.
Sheria
hiyo inaharamisha uhusiano baina ya watu wa jinsia moja na wale
watakaopatikana wanaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Marekani katika ajenda yake ya kupinga sheria hiyo mpya nchini Uganda.
Juma
lililopita Seneta mmoja kutoka Marekani ,Kirsten Gillibrand alilalmikia
vikali uteuzi wa waziri wa maswala ya kigeni wa Uganda Sam Kutesa
kuchaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Mataifa kutokana na kuwa anatokea
Uganda.
Marekani imeiwekea Uganda vikwanzo kuhusina na sheria ya wapenzi wa jinsia moja.
Watu 9000
walikuwa wametia sahihi pendekezo la kuitaka Umoja wa Mataifa kumng'oa
kitini bw Kutesa aliyechaguliwa licha ya kampeini hiyo.
Wanaharakati
wa wapenzi wa jinsia moja wameend mahakamani wakitaka sheria hiyo
iondolewe lakini inatarajiwa kupingwa kwani rais Yoweri Museveni
aliupitisha maksudi kudhihirishia wafuasi wake kuwa yu huru kutokana na
shinikizo kutoka kwa mataifa ya ughaibuni .
Punde
baada ya kupitishia kwa sheria hiyo mpya benki kuu ya dunia iliahirisha
utoaji wa mkopo wa dola milioni 90 ambazo zilikuwa zinapaswa kutumika
kuimarisha sekta ya Afya nchini Uganda .
Mataifa mengi tu ikiwemo Denmark, Norway, Uholanzi na Sweden zote zimekatiza msaada kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.
0 comments: