Mbali
na kuwa na afya tete, pia Jack anadaiwa kulalamikia haki za msingi za
kibinadamu ambazo anazikosa mahabusu kwa kuishi maisha kama ya mtu aliye
kifungoni.
Akizungumza
juzi jijini Dar, mtu anayejitolea kumpa msaada na kumtembelea Jack
mahabusu, Macau, China alikoshikiliwa, Matilda alisema Jack anaumia kwa
kupewa maisha kama tayari amehukumiwa, anaona bora hukumu yake ipite
ajue moja.
“Kiukweli Jack anaumwa, alishindwa hata kwenda mahamani, mbaya zaidi hata wakili wake naye hakutokea siku hiyo.
“Halafu
kule mahabusu anafanyishwa kazi ngumu ambazo hastahili kama mahabusu na
amesema hata watu wake wa karibu ambao anaamini kwa kipindi hiki
wangekuwa wanampa faraja hawaoni, anatamani angekamatiwa Bongo labda
kuna watu wanapenda kwenda kumtembelea kule Macau lakini hawana uwezo.
“Wabongo
wengi ambao wako Macau kwa ajili ya sanaa ya sarakasi ndiyo kidogo
wanakwenda kumtembelea siku mojamoja,” alisema Matilda.
Juni
20, mwaka huu, tulizungumza na Mbongo Fleva anayedaiwa ni mtu wa karibu
na Jack, Juma Khalid ‘Jux’ na kumuuliza kwa nini hajawahi kwenda
kumtembelea ‘bebi’ wake mahabusu kama wanavyofanya Wabongo ambao wako
Macau, akajibu:
“Sipendi kusikia ishu yoyote inayomuhusu Jack kwani nina mambo mengi ya kuongelea na si ishu za Jack kila kukicha.
“Kwa kipindi hiki sitahitaji mtu aniulize ishu za Jack, zinanitibua sana na kama kuongelewa zimeshaongelewa hivyo sioni kipya.”
Hii
ni mara ya tatu kwa Jack kupanda mahakamani, mara ya kwanza ilikuwa
Aprili 10, mwaka huu kosa likiwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni
aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 223. Mara ya pili ilikuwa Mei 23, mwaka huu.
0 comments: