Mheshimiwa
Mbunge Anne Kilango, muda mchache uliopita amejibu habari za Mkurugenzi
wa IPP Mzee Mengi kupiga marufuku magazeti yake kuandika habari za
Mbunge huyo na Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola, kwa kuwa upande wa Waziri
wa Madini na Nishati Prof. Muhongo katika vita ya Bilionea huyo na
Waziri Muhongo, Mheshimiwa Kilango amesema:- "Kama habari hizi ni kweli,
basi Mzee Mengi atakuwa amekosea kitu kimoja, mimi simuungi mkono
Muhongo kama Muhongo, natetea Serikali ambayo ndio wananchi na wala sio
vinginevyo" alimaliza na kukata simu!! |
0 comments: