MAHAKAMA KUU YA TANZANIA YATUPILIA MBALI KESI DHIDI YA WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA
Mahakama kuu ya Tanzania imetupilia
mbali kesi dhidi ya waziri mkuu, Mh. Mizengo Pinda iliyofunguliwa na
kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC na chama cha wanasheria
Tanganyika TLS kwa sababu hawana mamlaka kisheria ya kumshtaki. Kesi
hiyo iliyokuwa inasikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na
Jaji Kiongozi Fakih Jundu imetupiliwa mbali baada ya jopo hilo
kukubaliana na hoja za pingamizi zilizowasilishwa na Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali George Masaju.Kituo cha sheria na haki za binadamu na
TLS walimshtaki Waziri Mkuu Pinda pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kwa kauli aliyoitoa bungeni Juni 20 mwaka jana ya kuwataka polisi
kuwapiga watakaokaidi amri halali ya polisi.
Akisoma hukumu hiyo jaji Jundu huku akinukuu baadhi ya ibara amesema
Ibara ya 100 (2) inaweza kujadiliwa mahakamani, ambayo inasema bila
kuathiri katiba au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika,
Mbunge yoyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani
kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au
alilolileta bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.
Amesema kutokana na sababu hizo, mahakama inatupilia mbali kesi hiyo kwa
sababu waliofungua kesi, LHRC na TLS hawakustahili kisheria kufungua
kesi hiyo kwa sababu hawakuathirika.
0 comments: