BRAZIL 1 vs 0 SERBIA: FRED AWAOKOA, LAKINI MASHABIKI WAZOMEA KIWANGO `MBOFU MBOFU` YA SAMBA
Aliwaokoa: Fred aliifungia bao pekee Brazil katika pasha pasha ya kombe la dunia.
Fred akichukua mpira katika dakika ya 58 na kufunga bao kwenye uwanja wa Morumbi
Hana janja: Branislav Ivanovic akimtazama Fred, lakini hakuwa na la kufanya
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki waliofurika uwanjani waliwazomea
wachezaji wa Brazil baada ya Fred kufunga bao hilo pekee katika dakika
ya 58.
Mchezo huo ulilalia kwa Serbia ambao walitengeneza nafasi nyingi hususani kipindi cha kwanza, lakini walikosa umakini.
Brazil
walikoswa katika dakika ya 30 baada ya Aleksandar Mitrovic kupiga
kichwa cha hatari na kutoka nje kidogo na katika kipindi cha pili,
Milos Jujic aliwakosa baada ya mpira wake kugonga mwamba.
Hulk
alifunga bao katika dakika ya 73 lakini lilikataliwa baada ya mwamuzi
kuonesha alikuwa ameotea, lakini video za uwanjani zilionesha kuwa
mwamuzi hayakuwa sahihi.
Mechi
hiyo ya kirafiki ilikuwa ya mwisho kwa wenyeji Brazil kabla ya kucheza
mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia wiki ijayo katika uwanja wa
Corinthians arena .
Brazil
wanahodhi michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka
1950 na wapo kundi A na timu za Cameroon, Mexico na Croatia.
Kikosi
cha Brazil: Julio Cesar, Dani Alves (Maicon 71), Luiz, Thiago Silva,
Marcelo (Maxwell 74), Gustavo, Paulinho (Fernandinho 64), Oscar (Willian
46), Hulk, Fred (Jo 75), Neymar.
Wachezaji wa akiba: Jefferson, Dante, Henrique, Ramires, Hernanes, Bernard, Victor.
Goli: Fred 58.
Kikosi
cha Serbia: Stojkovic (Lukac 88), Basta (Tomovic 86), Ivanovic,
Aleksandar Mitrovic, Kolarov, Dusko Tosic, Matic, Jojic, Tadic (Zoran
Tosic 69), Petrovic (Mrdja 86), Markovic (Gudelj 81).
Wachezaji wa akiba: Pejcinovic, Djuricic, Stefan Mitrovic, Ljajic, Bisevac, Vulicevic, Lazovic, Brkic.
Jembe: Neymar (kulia) akichuana vikali na mchezaji wa Serbia Dusan Basta
Huendi fundi: Mshambuliaji wa Brazil, Neymar akizuliwa na beki wa Chelsea, Ivanovic.
Mashabiki wa Brazil wakiishangilia timu yao katika mchezo wa mwisho wa kirafiki kuelekea kombe la dunia.
Walikosa uzalendo: Mashabiki wa The Sao Paulo waliwazomea wachezaji wao baaada ya kuonesha soka bovu kipindi kizima cha kwanza.
Ujumbe: Wachezaji wa Serbia wakiwa wameshikilia bango linalosomeka `Serbia inahitaji msaada` kabla ya kuanza kwa mechi.
0 comments: