208 wafariki kutokana na Ebola Guinea
Maafisa
wa afya duniani wanaarifu kuwa watu wasiopungua 208 wameaga dunia
kutokana na virusi vya Ebola nchini Guinea baada ya ugonjwa huo kusambaa
kwa siku za hivi karibuni.
Angaa
watu 21 waliaga dunia na visa vingine 37 vinavyohusiana na Ebola
kuripotiwa kati ya tarehe 29 mwezi Mei na tarehe 1 mwezi Juni na
kufikisha idadi ya visa hivyo kufikia 328 katika taifa hilo lililoko
magharibi mwa Afrika.
Hadi sasa, hakuna dawa za kuzuia wala kutibu Ebola- moja kati ya
virusi hatari sana duniani.Kati ya visa hivi, 193 vilithibitishwa
kupitia vipimo vya maabara.
Zaidi ya nusu ya vifo vya hivi karibuni vilitokea kusini mwa eneo la Guekedou, mahali ambapo ugonjwa huo ulianzia.
Visa vitatu vimedhibitishwa na vingine 10 vinavyodhaniwa kuwa wa ugonjwa huo vimeripotiwa katika nchi Jirani ya Sierra Leone.
Inaaminika kuwa watu kumi wameaga dunia katika taifa hilo, huku wengine kumi wakifariki nchini Liberia.
Wanaotoa
misaada ya matibabu wamesema kuwa sababu moja ya ongezeko la ugonjwa huo
ni kuwa watu wanakataa kwenda hospitalini kutibiwa na badala yake
kuwaendea waganga.
Homa hiyo
ina uwezo ya kuuwa hadi asilimia 90 ya walioathiriwa na huambukizwa
wakati maji maji ya mwili, kama vile damu, mkojo na jasho la mtu au
mnyama aliyeambukizwa yanapogusana na ya mtu mwingine.
Hata hivyo, binadamu wana nafasi nzuri ya kupona iwapo ugonjwa huo utatambuliwa mapema na kupata matibabu.
Wataalamu
kutoka shirika la afya ulimwenguni pamoja na madaktari wasio na mipaka
wanaofanya kazi katika eneo hilo wanachunguzwa baada ya uwezekano wa
kuathiriwa na Ebola.
0 comments: