NUSU MWAKA UMEFIKA, JE MALENGO YAKO YAMEFIKIA WAPI?
Ungwe
ya kwanza ya mwaka 2014 inamalizikia, naamini ulikuwa na vitu ambavyo
ulidhamiria kuvifanya mwaka huu. Sasa ni wakati wa kujaribu kupitia je
mambo yako au mipango yako imefikia wapi na je unaendelea vizuri au
vibaya? Ni vizuri kufuatilia mambo yako yanavyokwenda wakati nusu ya
kwanza inaenda kuisha na tunatarajia kuingia nusu ya pili hivi karibuni.
Unapoangalia
nyuma ulikotoka kitu cha kujichunguza ni mafanikio gani uliyopata
miezi mitano inayoishia na hasara gani au vikwazo ulivyokutana navyo na
unajirekebishaje unapokwenda nusu ya mwisho kwenye mwaka 2014?
Uchumi wako unakwendaje?
Je
mwenendo wa fedha zako unakwendaje katika nusu hii ya kwanza? Matumizi
yako na mapato yanaendana? Je umetengeneza madeni mengi au umeweza
kuweka akiba kwa ajili ya baadaye? Kama ulipanga kuanzisha mradi hebu
angalia kama mradi umeanza na kama haujaanza ujiulize tatizo ni nini?
Je kwenye mahusiano yako yanakwendaje?
Ni
vizuri kujua mahusiano yako yanaendeleaje na kama yana mwelekeo
unaostahili.Kam umekuwa unazunguka na watu sahihi inawezekana mahusiano
yako yakawa yenye tija ila kama umekuwa na watu ambao sio sahihi
hujachelewa kujiondoa na kujitenga nao. Kumbuka maisha yako ya baadaye
yanakuhitaji ufanye maamuzi sahihi ili usipate majuto baadaye.
Taaluma yako je?
Hebu
fuatilia kitaaluma unaendeleaje na umeweza kufanikisha kitu gani katika
kipindi hiki. Je kuna kitu ulipaswa kufanya na hakijafanyika? Kama
ulipanga kujiendeleza je umeweza kuchukua hatua yeyote?
Imani yako ikoje?
Mara
nyingi watu wengi huiweka mbali imani wakifikiri ni ushamba au ujinga
ingawa wanaiihitaji. Unaweza kusema huna imani lakini kuna kitu
unakiamini ambacho kinaweza kuwa ni sahihi au sio sahihi. Lazima ujue
kwa miezi hii sita inayoishia ukoje kiimani? Hata kama una biashara vile
vile ujue namna biashara yako inavyokwenda, je inakuwa au inashuka?
Ongeza ubunifu na weledi katika kila unachokifanya.
0 comments: