MADAKTARI WAKUNA VICHWA KUREJESHA AFYA YA MTOTO NASRA ALIYEISHI KWENYE BOX MIAKA 4
Nasra akiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
MTOTO
mwenye umri wa miaka minne aliyefungiwa ndani ya boksi kwa zaidi na
miaka mitatu mkoani Morogoro, amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi na tiba zaidi huku wataalamu
wakikuna vichwa namna ya kumrudishia afya yake. Imeelezwa
jopo la madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ya binadamu wakiwemo
wataalamu wa saikolojia, wanahitajika kwa ajili ya kumwezesha mtoto huyo
mwenye ulemavu kuwa katika hali ya kawaida.
Aidha, pamoja na uhitaji wa jopo la wataalamu hao, mtoto huyo ambaye
amelazwa katika wadi ya watoto, atahamishiwa katika wadi maalumu ya
watoto wenye utapiamlo awe karibu na uangalizi wa lishe baada ya
kubainika ana udhaifu mkubwa wa lishe.
Wakizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam kwa nyakati
tofauti hospitalini hapo, Daktari Bingwa wa Watoto wa MNH, Dk Mwajuma
Ah- mada alisema mtoto huyo hajazidiwa kuumwa.
Alisema walimpokea juzi usiku na hatua za awali zilizofanywa ni pamoja na kuchukua baadhi ya vipimo kwa ajili ya uchunguzi.
“Mtoto aliletwa hapa jana (juzi) usiku, baadhi ya vipimo vimechuku-
liwa, vingine atafanyiwa leo (jana) ikiwa ni pamoja na kumfanyia huduma
ya kum scan (kumwingiza kwenye mashine maalumu) mwili mzima ili tufahamu
tatizo na tiba sahihi,” alisema Dk Ahmada.
Alisema huduma ya tiba kwa mtoto huyo siyo ya daktari bingwa mmoja
bali inahitaji jopo la wataalamu waki- wemo wa mifupa, saikolojia,
viungo na magonjwa mbalimbali ya binadamu kumsaidia mtoto huyo.
“Kwa sasa hatuwezi kusema lolote kubwa kuhusu mtoto huyo ndio kwanza
kafika na ndiyo tuko kwenye hatua ya awali ya kuchukua vipimo, na leo
atafanyiwa huduma ya kumulikwa mwili mzima ili tujue tunaanzia wapi”,
alisema Dk Ahmada.
Alisema pamoja na kusubiri majibu ya vipimo, hatua wanayochukua ni ya
kumhamishia kwenye wadi ya watoto wenye utapiamlo, ili kutibu maradhi
hayo ambayo ndio yameonekana awali, kwani mtoto amekosa lishe na viru-
tubisho muhimu vya awali.
Alifafanua, katika hatua hiyo ya awali, mtoto huyo atakuwa akipewa
maziwa ya lishe na kuendelea na tiba ya dawa za kuua vijasumu kutokana
na kusumbuliwa na vichomi.
Akizungumzia kwa ufupi ikiwa mtoto huyo anaweza kurejea katika hali
ya kawaida kwa viungo kunyooka na kutembea, Dk Ahmada alisema pamoja na
kusubiri majibu ya vipimo, lakini pia tiba ya mtoto inategemea zaidi
historia ya mtoto mwenyewe.
Mlezi azungumza Kwa upande wake, mlezi wa mtoto huyo , Josephina Joel
akizungumza na gazeti hili wadini hapo alisema mtoto anaendelea vizuri
ingawa juzi alikuwa na homa.
Hata hivyo alisema imeshuka, na kwamba kadri siku zinavyosonga, anaona uchangamfu wa mtoto.
0 comments: