JE SARATANI YA TEZI-KIBOFU NI"MARADHI YA ZINAA ? " SOMAAA KUJUA ZAIDI HILI TATIZOO

Ingawa
baadhi ya Saratani husababishwa na maradhi fulani fulani, kitengo cha
utafiti wa Saratani nchini Uingereza kinasema kuwa ni mapema mno
kuongeza Saratani ya tezi kibofu kwa Saratani hizo.
Wanasayansi waliofanya utafiti huo walichunguza celi za tezi kifobu cha binadamu katika maabara.
Waligundua kuwa maradhi ya zinaa yaitwayo, 'Trichomoniasis' yalichochea ongezeko la Saratani hiyo.
Hata hivyo mfumo wa maisha pia unachangia ongezezeko la visa vya magonjwa ya Saratani.
Ugonjwa
wa 'Trichomoniasis' unaaminika kuwaathiri watu milioni 275 duniani na
moja ya maradhi maarufu ya Zinaa ambayo hayasababishwi na Virusi

'Dalili za Trichomoniasis'

'Dalili za Trichomoniasis'
Kawaida, mtu hatapata dalili za ugonjwa huo na inawezekana asijue kama anaugua ugonjwa huo.
Wanaume
huhisi kujikuna sana ndani ya uume wao , kupata hisia za kuchomeka
wakati wanapokwenda haja ndogo au kuvuja majimaji meupe kutoka kwa uume
wao.
Wanawake pia wana hisia tu sawa na hizo katika sehemu zao za isiri pamoja na kuwa na harufu mbaya.
Utafiti huu wa hivi karibuni sio wa kwanza kuhusisha ugonjwa wa 'Trichomoniasis' na Saratani ya Tezi kibofu.
Utafiti
uliofanywa mwaka 2009 ulipata kuwa robo ya wanaume walio na Saratani
hio walikuwa na dalili za ugonjwa wa Trichomoniasis na wanaume hawa pia
walikuwa na uvimbe ambao ulikuwa umekomaa mno.

'Hoja ya Uchunguzi zaidi'
Uchunguzi huo pia unaonyesha njiaambazo ugonjwa huo wa zinaa unawaweka wanaume katika hatari ya kupata Saratani ya tezi kibofu.
Profesa
Patricia Johnson na watafiti wenzake, waligundua kuwa viini
vinavyosababisha ugonjwa wa 'Trichomonas vaginalis' - huvuja proteni
ambayo husababisha Saratani ya Tezi Kibofu kuzuka.
Mtaalamu
wa afya, Nicola Smith,anasema uchunguzi huu unaonyesha tu njia ambazo
ugonjwa wa zinaa wa Trichomonas vaginalis unazidisha uwezo wa mtu kuugua
Saratani ya Tezi Kibofu na kuchochea seli kukuwa kwa kasi.
"Lakini
uchunguzi huu ulifanywa tu katika maabara na matokeo ya awali kwa
wagonjwa yalikosa kuonyesha uhusiano kati ya ugonjwa huo na Saratani ya
Tezi Kibofu,'' alisema Bi Nicola
Kwa
kauli hii wanasema kuwa uchunguzi zaidi unahitajika ili kuabini hasa
kinacho sababisha Saratani ya Tezi kibofu kwani ugonjwa wa
Trichomoniasis husababisha tu mazinigira kwa ugonjwa huo kukomaa ila sio
chanzo cha ugonjwa wenyewe.
0 comments: