UTAFITI: UTUMIAJI ULIOZIDI WA SIMU KWA WAZAZI HUPUNGUZA UKARIBU NA WATOTO WAO
Watafiti
kutoka Boston Medical Centre wamebaini kuwa matumizi yaliozidi ya simu
kwa wazazi hupunguza mapenzi kutoka kwa watoto wao.
Katika
utafiti waliofanya, waligundua kuwa mmoja kati ya wazazi watatu hutumia
simu mara kwa mara wakati wa chakula na huku utafiti mwingine ukidai
kuwa kukosekana kwa kutazamana machoni na mazungumzo ya kawaida
hupunguza ukaribu na watoto wao.
Katika
utafiti huo waligundua tabia tano za wazazi kuanzia wazazi wasiotumia
kabisa simu zao wakati wa chakula, wazazi wanaoweka simu zao mezani bila
kuzitumia, wazazi wanaotumia simu mara chache wakati wa kula, wazazi
wanaotumia simu baada ya chakula na wale wanaotumia simu muda wote.
Watafiti
hao wamebaini kuwa pale wazazi wanapotumia muda mwingi kuangalia simu
zao, watoto wao huanza kufanya fujo kutaka attention.
“Wazazi wanaojikuta wakitumia sana simu zao wanaonekana kuwa na maongezi hafifu na watoto wao,” alisema Dr Jenny Radesky
0 comments: