AFYA:JE WEWE NI MJAMZITO AMA UNATARAJIA KUSHIKA MIMBA? KIJUE KISUKARI CHA MIMBA-(GESTATIONAL DIABETES)


leo paparazihuru nimeamua kuwaletea Gestational diabetes/kisukari cha wakati mama akiwa mjazito kwahiyo kama tiyari shemeji akukojolea huko chini basi hii inakuhusu.....na kama unamatarajio hayo soma hii ni muhimu mno !!!!!!!!!. 


Hii condition hutokea pale sukari katika damu ya mama mjamzito ikipanda juu. Sukari hiyo katika damu, hupanda juu kutokana na hormone kubadilika katika mwili wa mama na kusababisha kisukari cha mimba. Ijapokuwa sukari inakuwa juu kwenye mwili haifikii kiwango cha kumsababishia mama mjamzito kuwa na ugonjwa wa kisukari.

Ni matatizo gani yanayoweza kumtokea mama/mtoto kama mama aki-end up na kisukari cha mimba?
Well, katika ile miezi mitatu ya mwanzo, kisukari kinaweza kufanya mtoto akazaliwa na matatizo ya akili ama moyo. Pia mama anaweza kupata miscarriage.



Mama akiwa katika second na third trimester, kama mama anakisukari cha mimba, huweza kumfanya mtoto awe mkubwa kupita kipimo kinacho takiwa na hivyo kusababisha matatizo kwa mama wakati anapojifungua. Na pia mtoto kupata trauma wakati anapokuwa akitoka tumboni. Pia kutokana na kwamba mtoto anapokuwa tumboni alikuwa anapata dozi kubwa kutoka kwa mama ya insulin anapotoka tumboni kisukari cha mtoto huweza kushuka mpaka kiwango cha chini kabisa kutokana na kwamba ameshatoka tumboni mwa mama na hana tena supply ya ile dozi kubwa ya sukari aliyokuwa akipata kutoka kwa mama hivyo kufanya sukari yake ya mwili kushuka chini gafla.

 Mtu wa aina gani ndo anaweza kupata kisukari cha mimba/gestational diabetes?

  • mama aliyeko overweight (mzito kuliko anavyotakiwa) kabla hajawa mjamzito
  • ethnic group kama ya watu weusi, wengi wako kwenye high risk ya kupata kisukari cha mimba
  • kuwa na sukari kwenye mkojo
  • kama sukari ya kwenye damu iko high mara kwa mara ijapokuwa mtu hata ugonjwa wa kisukari mtu bado huwa katika risk kubwa ya kupata kisukari cha mimba
  • kama kwenye familia kuna historia ya ugonjwa wa kisukari (watu kuwa na kisukari)
  • kama mama ameshawahi kuzaa watoto wakubwa sana previosly


Mama atajuaje kama ana kisukari cha mimba?
mara nyingi mama anapokwenda kufanya checkup toka mimba bado ni changa ndo doctor hufanya checkup ya kisukari. Hii checkup hushauriwa na doctor kwamaana doctor hawezi kumwangalia tuu mama na kuhisi ana kisukari cha mimba lazima first watamcheki mama damu and then wakiona levels za sukari katika damu hazija kaa sawa basi wanakushauri kufanya hiyo check ya gestational diabetes. 

Diet ni muhimu iwe nzuri kabla ya mimba na even wakati mama ni mjamzito. Kula diet nzuri isiyo na macarbohydrates mengi ndo inayosaidia haswa kutopata kisukari na hata kisukari cha mimba.





0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/