ULIONA PICHA ZA OMMY DIMPOZ ALIVYOKAMATWA NA POLISI HUKO LONDON??? BASI CHEKI PICHA HAPA
Ommy Dimpoz ambae amerudi nchini hivi karibuni kutoka London ambapo alikua ameenda kwa ajili show 2 na kushoot Video chini ya usimamizi wa Gonga Entertainment. Katika Picha Ommy Dimpoz
anaonekana ameshikiliwa na Metropolitan Police wa nchini uingereza na
hii ni moja kati ya scene ambayo imetumika katika Video ya Nyimbo yake
mpya iliyotengenezwa na Director Mr Moe Musa ambaye amefanya kazi nyingi sana na kubwa za wasanii wa Uingereza na Nigeria kama Azonto ya Fuse ODG.
Video hii
inatarajiwa kumalizika na kuachiwa mwishoni mwa mwezi huu ambayo
inatarajiwa kuwepo kwenye chanel nyingi na kubwa kutokana na Director na
ufanyaji wa Video hii ambapo vifaa vilivyotumika ni modern na vyenye
gharama ya juu sana ikiwemo Camera RED pamoja na professional FILM crew waliotumika kushoot video hii.
Video hii imemgharimu OMMY Dimpoz si chini $20,000
za kimarekani ambazo ni kiasi pekee alichomlipa Director huyo na hiyo
ukitoa gharama zake nyingine zilizotumika kwenye kusafiri pamoja na
kuwepo nchini Uingereza kwa kipindi kizima cha utengenezaji wa video hiyo.
0 comments: