SITTA ASIPOACHA MAMBO HAYA HATUNA KATIBA MPYAAA .. JE WAYAJUA NI NINI SOMA HII
WAZIRI wa Afrika Mashariki Samuel Sitta ameweka historia nyingine
mpya katika maisha yake, baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa
Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum la Katiba Mpya inayoendelea jijini
Dodoma.
Sitta ameshinda kwa kura 487 sawa na asilimia 87.7 huku mpinzani wake Hashimu Rungwe akipata kura 69 12.3% ya kura zote zilizopigwa,jumla ya kura zilizopigwa ni 629 huku zilizo haribika ni 7.
Sitta ambaye aliweza kuwateka watanzania na kujipatia umaarufu mkubwa wakati akiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akiwa na kauli mbiu ya kuendesha Bunge hilo kwa spidi na viwango ndiye muhimiri mkuu katika Katiba Mpya hivi sasa.
Sitta alianza kuvuma zaidi na kuonekana shujaa machoni mwa watanzania baada ya kuunda kamati ya Bunge iliyokuwa chini ya Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe pamoja Injinia Stela Manyanya ambayo ilimn'goa madarakani aliyekuwa Wazirikuu Edward Lowassa.
Wakati huo maamuzi ya kamati hiyo ilioeneka kuwa ya busara machoni mwa watanzania kutokana na ufisadi ulioibuliwa katika mradi wa uememe wa dharura kupitia kampuni ya kufua umeme ya Richmond.
Miaka mitano baadaye ilibainika kwamba hakukuwa na ufisadi wa kutisha katika mradi huo badala yake mambo yaliendeshwa kishabiki na chuki huku Lowassa akionekana shujaa machoni mwa watanzania. kiasi ambacho Chama Chake Cha CCM kikaamua kumfungia yeye pamoja makada wengine sita kujishugulisha na siasa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Sababu kuwa iliyofanya CCM kuwafungia makada hao ni kwamba wameanza kutengeneza mazingira ya kufanya kampeni za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kabla ya muda huku ikiwa ni kinyume na kanuni za Chama hicho, hata hivyo wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kwamba hizo ni njama za kumzuia Lowassa kuwania urais kupitia CCM kwa hufu kwamba hivi sasa anakubalika na ana nguvu tofauti na kipindi ambacho Sitta akiwa Spika.
Leo Sitta amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kudumu la Bunge Maalum la Katiba Mpya, kwa kura nyingi na kumshinda mpinzani wake Hasimu Rungwe.
Ni wazi kwamba Sitta alikuwa na nguvu ya kupenya katika nafasi hiyo kwasababu ana sifa vigezo,uwezo na uzoefu wa kuendesha shuguli za bunge, hasa katika kipindi hiki ambacho bunge limegubikwa na vurugu vijembe na vituko vya kila namna.
Kutokana na sifa hizo kila mtanzania hana shaka kabisa na uteuzi wa Sitta kushika nafasi hiyo, ila anachangamoto kubwa katika kazi hiyo kwa sababu anapaswa kuliongoza bunge hilo kwa kufuata kanuni za bunge hilo huku akiweka maslahi ya CCM nyuma badala yake aweke maslai ya watanzania na Taifa kwa ujumla mbele yake, huku akikwepa kufanya maamuzi ya chuki na ushabiki kama ilivyotokea wakati akiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Lakini pia anakabiliwa na changamoto za kutatua suala la kura za aina gani zinapaswa kutumika katika Bunge hilo, kwani mpaka anachaguliwa suala hilo halikuwa na mwafaka wowote baada ya CCM kung'ang'ania kura za wazi huku wabunge wengine kutoka upinzani pamoja wabunge wateule wa rais kutaka kura za siri lakini pia suala la kura za siri ndiyo mwongozo ulioko katika Katiba ya sasa.
Labda ni mkumbushe Sitta jambo moja kwamba yeye ni mmoja kati ya watu wanaowania urais wa tanzania ingawa rungu la CCM dhidi ya wakina Lowassa na rafiki yake Bernard Membe haikumgusa na kama kweli anamipango hiyo, basi awape watanzania katiba itakayojibu maswali yao kuhusu umaskini lakini kama kweli yeye ni kibaraka wa Membe kama anavyo nyoonshewa kidole na baadhi ya watu najua kabisa ataenda kufanya madudu ili kumfurahisha Membe na CCM yake.

0 comments: