MICHEEPUKO NOMA!!! ATEMBEZWA KAANGA MOKO KISA FUMANIZI!!!



OMBA usifumaniwe! Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Salum Athuman (22), amejikuta akivishwa khanga na kutembezwa mitaani baada ya kwenda nyumbani kwa mwanaume mwenzake, Dastun Mkereti (26) kwa lengo la kujivinjari na mke wa mtu, Stela Ramadhan (20), akafumaniwa.

Tukio hilo lililofunga mitaa lilijiri maeneo ya Temeke, Dar, hivi karibuni na kugeuka sinema ya bure.

Kama ilivyo ada, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kilichopania kutokomeza maovu nchini, wiki hii kilitinga maeneo hayo baada ya kutonywa na Mkereti kwamba kuna njemba anamsumbua mkewe. 

Alidai kuwa jamaa huyo amekuwa akimsumbua mkewe kwenye simu kwa kutaka waonane ili wavunje amri ya sita huku akijua fika kuwa Stela ni mke wa mtu na alishapewa onyo mara nyingi na mwenye mke. 

Alifunguka kuwa cha kushangaza, pamoja na mwanamke huyo kubadili namba ya simu, wiki iliyopita jamaa alimpigia Stela kisha akamsisitiza waonane, ikibidi alale naye siku nzima kwa kuwa alikuwa anataka kukumbushia enzi zao kwa sababu aliwahi kutoka naye kimapenzi, kipindi cha nyuma kabla hajaingia kwenye ndoa. 

Mkereti alisema kwamba baada ya kuona ndoa yake iko shakani kutokana na pepo la usaliti kumnyemelea mkewe, alimwambia mama watoto wake amruhusu kidume huyo waonane, ikibidi wakutane nyumbani kwake kwa kumdanganya kuwa haishi naye kwa sasa japo ndoa yao bado changa. 

Alitiririka kwamba bila woga, njemba huyo alimpigia simu Stela na kumtaka amuelekeze kwake ili afike na kujiachia ‘kimalavu’ siku nzima. 

Mkereti ambaye ni mfanyabiashara, alisema siku hiyo hakwenda kusaka ‘bingo’ ili kumwekea mtego ‘mwizi’ wake aliyemsumbua kwa muda mrefu. 

Wanandoa hao, wakiwa ndani wakimsubiri mgeni wao, mishale ya saa 8:00 mchana ndipo jamaa akatinga akiwa amepigilia pamba kali kwa lengo la kumshawishi bishosti huyo aisaliti ndoa yake bila kujua mumewe alikuwepo. 

Alifunguka kwamba Salum alipofika, Stela alimkaribisha na kuketi huku yeye (Mkereti) akiwa amejibanza chobingo. 

Alisema alimshuhudia mgoni huyo akijinafasi na kutawala nyumba kama kwake huku akidai chakula na kukumbushia ombi lake la kulala na Stela siku nzima. 

Baada ya mambo kukaa sawa, ndipo Mkereti akawashtua OFM waliokuwa wanaujua mchezo.
Wakati jamaa akiwa tayari amesaula tayari kwa mchezo ndipo Mkereti na OFM wakamfuma laivu.
 

Kwa kushirikiana na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Gido Herman pamoja na majirani wa wanandoa hao, walimhoji jamaa huyo kwa nini amekuwa akimsumbua Stela, akatoa ufafanuzi wake. 

“Jamani naomba mnisamehe, sina sababu yoyote lakini mimi na Stela tulipendana sana kipindi hicho, sikujua kama nimewekewa mtego.” 

Hata hivyo, Mkereti aligoma kumwachia au kumpeleka Salum kituo cha polisi tangu mchana hadi saa 3:00 usiku alipomtoa kisha akafungwa kanga na kuanza kumtembeza mitaani hadi polisi.
Wakiwa mitaani, watu waliojitokeza kushuhudia kituko hicho walikuwa wakimwimbia jamaa huyo nyimbo za kuudhi.”

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/