HATMA YA JIMBO LA KALENGA KUJULIKANA LEO


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh.Jaji Mst.Damian Lubuva ametoa wito kwa wananchi walio jiandikisha Kupiga Kura Katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kalenga utakao fanyika tarehe 16 machi 2014, Kujitokeza kwa wingi kwenda kwenye Vituo vilivyopangwa kwa ajili ya Kupiga Kura ili kutekeleza haki yao ya katiba ya kumchagua mtu anayemtaka kuwa kiongozi wao.
Jaji Mst.Lubuva amesema, vituo vya kupiga kura vitafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi jioni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewakumbusha wananchi wa Kimbo la Kalenga kubeba Kadi ya Mpiga kura kwa kuwa bila ya kadi ya Mpiga kura hatoruhusiwa kupiga kura.
Ameongeza kuwa, wagonjwa wanaoishi na ulemavu wa aina mbalimbali, wanawake wajawazito, wanaonyonyesha na wazee hawatatakiwa kujipanga kwenye mstari bali wataelekezwe kwenda moja kwa moja kupiga kura.
Amesema, mpiga kula anayeishi na ulemavu wa kutoona ataruhusiwa kuja kituoni na mtu aliyemchagua mwenyewe, na mtu mmoja anaweza kumsaidia mpiga kura mmoja tu, labda kama wapo wapiga kura zaidi ya mmoja kutoka katika familia moja.
Aidha, Tume imesisitiza mambo muhimu vikiwemo vyama vya siasa kuweka mawakala wake katika vituo vyote 216 vya kupiga kura na kujumlisha kura pamoja na mawakala kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
Ameongeza kuwa mpiga kura anatakiwa kupiga kura katika kituo alichoandikishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuzingatia maadiri mara baada ya mpiga kura kupiga kura anatakiwa kurejea nyumbani kwa kuwa vyama vya Siasa vitakuwa vimeweka mawakala wake ambao watalinda maslahi ya vyama husika na wagombea wao.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inamtaka mtu kupiga kura kwa Siri na asishawishiwe na mtu yoyote kueleza nani amempigia kura na ni kosa la Jinai kumkataza mtu kwenda kupiga kura kwani ni haki yake ya kumchagua mtu anayemtaka kuwa kiongozi wake.
Matokeo hayo ya Uchaguzi utakaofanyika kesho 16 machi 2014 yatatangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi huo.
Hata hivyo tume inamatumaini yakuwa hali ya amani na utulivu ambayo imekuwepo hadi sasa, itaendelea kudumishwa.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/