ALIYEDONDOSHA BOMU LA NYUKILIA HIROSHIMA AFARIKI DUNIA


kapteni Theodore Van Kirk, katikati, na wenzake wakati wakirejea kutoka katika misheni ya Hiroshima, Japan Agosti 6, 1945. Kushoto kwake ni Kanali Paul Tibbetts kamanda wa msafara.
MWANAANGA wa mwisho katika  ndege aina ya B-29  (Enola Gay) iliyopiga mji wa Hiroshima uliopo Japan  na bomu la nyukilia (“Little Boy”) mji wa Hiroshima, amefariki dunia.Kwa mujibu wa The Atlanta Journal-Constitution,Mwanaanga huyo Theodore “Dutch” Van Kirk, 93, alikuwa navigeta  wa ndege hiyo ambayo Agosti 6 1945 ilidondosha bomu hilo na kumaliza vita vya dunia.
Van Kirk

Baada ya kifo cha   Morris Jeppson, mwaka 2010,Van Kirk alikuwa ndiye mpiganaji pekee aliyebaki kati ya wapiganaji dazeni walishiriki katika misheni hiyo.
Kwa miaka mingi alikuwa akiishi katika makazi ya wastaafu  huko Stone Mountain na walikuwa akiishi na James Starnes,  navigeta wa USS Missouri ambaye alipokea ujumbe wa kujisalimisha rasmi kwa Japan, Septemba 2, 1945.
Starnes, amesema rafiki yake alikufa Jumatatu baada ya kuwa hospitalini kwa wiki kadhaa.
Alisema kwamba kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi alidondosha chozi kwa rafiki yake huyo ambaye kwa pamoja kwa nyakati tofauti walikuwepo wakati wa kuandika historia ya dunia.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/