MSANII MWINGINE KUTOKA TANZANIA AKAMATWA NCHINI CHINA
Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.
HUKU modo
maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota
jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga),
mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki
wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na
polisi nchini humo.
Tukio
hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako
maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong,
China.
JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa
mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma
Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye
Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika
kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa
madawa ya kulevya nchini China.
'Winnie Mandela' wa muziki wa kizazi kipya Bongo akiwa chini ya ulinzi mkali China.
MADAI YA KUBEBA UNGA
Ilidaiwa
kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa kubeba
mzigo wa unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani kuelekea
kituo cha polisi.
APITA VIZUIZI, AKAMATWA
Ilisemekana kwamba Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar,
alifanikiwa kupita vizuizi vyote lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini
humo ndipo akajikuta akikamatwa na kutembezwa mtaani kama mhalifu wa
kivita.
“Unaambiwa ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha
za kutisha sana. Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna
Wabongo wengi hapa Hong Kong,” kilisema chanzo chetu kutoka Hong Kong.
Ilidaiwa kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye
kitengo cha kudhibititi madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa
nchi hiyo imechafuka kwa uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo
limeifanya serikali ya China ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha
wanatokomeza wimbi hilo.
KWA WABONGO CHINA
Chanzo chetu kilisema kwamba kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa
China wanaishi kama digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha
pasipoti zao na hata wengine wanadiriki kukataa uraia wao kwa kuwa
Wabongo ndiyo wanasakwa kwa wingi.
“Sasa hivi jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani
ndiyo wenye sifa ya uingizaji wa dawa za kulevya nchini China,”
kilisema chanzo hicho na kuongeza:
KAMA HUAMINI MUULIZE JUX AU PETIT MAN
“Hicho ndicho kilichomtokea Winnie. Nakwambia Wabongo wanazidi kukamatwa na madawa ya kulevya. Yaani ni aibu, huwezi kuamini.
“Wabongo wengi sana wamekamatwa Hong Kong na wengine familia zao Bongo hazijui.
“Kama Watanzania hawaamini wawaulize Jux na Petit Man ambao walishuhudia mtiti mwanzo mwisho.”
BALOZI WA TANZANIA CHINA
Ili kupata undani na idadi ya Watanzania wanaokamatwa kwa ishu za
madawa ya kulevya nchini China, gazeti hili lilimtafuta Balozi wa
Tanzania China, Luteni General Abraham Shimbo ambapo simu yake ya
ofisini iliita bila kupokelewa. Wakati Jack Patrick akisubiri
kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine mwezi ujao, ripoti zinaonesha
kwamba wapo Watanzania wengi waliofungwa na wengine kunyongwa kwa msala
wa madawa ya kulevya.
0 comments: